Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imesaidia ujenzi wa darasa kwa
ajili ya watoto wenye ulemavu katika shule ya msingi Pongwe iliyopo
nje kidogo ya Jiji la Tanga.Darasa hilo limejengwa ikiwa ni jitihada
za kampuni hiyo kusaidia maendeleo ya elimu nchini kupitia mpango wa “
Tunakujali” unaohusisha wafanyakazi wake kuchangia katika shughuli za
kijamiiMkurugenzi wa Huduma za jamii wa kampuni ya Airtel Bi Adriana
Lyamba amefanya ukaguzi wa ujenzi huo na kuahidi kuendelea kusaidia
mpango wa elimu kwa makundi yenye mahitaji muhimu hapa nchini.
Bi
Lyamba amesema kuwa msaada huo umetokana na mahitaji ya miundombinu
kwa jamii ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwenye shule hiyo ambayo
kwa Jiji la Tanga ndiyo inatoa elimu kwa watu wenye ulemavu.“sisi
Airtel tumeona umuhimu wa wanafunzi wenye ulemavu na tumetambua
mahitaji yao ndio maana tumekuja na mpango huu wa ujenzi wa Darasa
hapa Pongwe” alisema Bi Lyamba.
“ujenzi wa Darasa hili ni sehemu ya
mpango wetu wa kusaidia ukuaji wa elimu hapa nchini kupitia kampeni
yetu ya shule yetu na tunaamini utasaidia makundi yote ya jamii”
aliongeza Bi Lyamba.Mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Bw. Mfaume
Kamba amesema, msaada huo wa ujenzi wa chumba hicho utasaidia sana
kupunguza tatizo la wanafunzi wenye mahitaji maalumu kukosa sehemu ya
kujifunzi.
Bw. Mfaume amesema, Jengo hilo ni msaada mkubwa kwa
wanafunzi wa awali kwenye shule hiyo ambao kwa muda mrefu wamekuwa
wakisomea nje kutokana na kutokuwepo kwa chumba cha kusomea.“msaada
huu ni mkombozi kwetu kwani kwa sasa wanafunzi wetu wa awali watakuwa
na mahala pazuri kwa kusomea na kuondokana na adha ya kujifunza wakiwa
kwenye mazingira ya nje” alisema Bw. Mfaume.
Shule hiyo ya Mchanganyiko
ya msingi ya Pongwe bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni
pamoja na ukosefu wa vyumba vya kutosha vya kujifunzi kwa watu wenye
ulemavu na vifaa vyake.
Wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakiongozwa
na Mkurugenzi wa Huduma kwa Jamii,Bi. Adriana Lyamba kubeba mabati kwa
ajili ya kupaua darasa litakalotumiwa na wanafunzi wenye ulemavu
kwenye shule ya msingi pongwe jijini tanga.
Mwalimu Mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi Pongwe, Mfaume Kamba
akitoa maelezo ya ujenzi wa darasa linalojengwa kwa msaada wa kampuni
ya simu ya airtel Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa kampuni hiyo,Bi. Adriana Lyamba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...