Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Wananchi limewakamata Wahamiaji haramu 64 raia wa nchi ya ETHIOPIA (Wahabeshi) katika Kijiji cha KIDOKA, Kata ya KIDOKA, Tarafa ya GOIMA, Wilaya ya na CHEMBA na Mkoa wa DODOMA, mmoja kati yao alikutwa akiwa amefariki dunia aliyetambuliwa kwa jina moja la TAJIRU anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 – 30. Watu hao walikuwa wakisafirishwa kwa Lori lenye namba za usajili T.353 AYW Mitsubishi Fuso lililokuwa likiendeshwa na OTHMAN YUNUS MTEKATEKA, miaka 45, na Mkazi wa ILALA Jangwani jijini Dar es Salaam akitokea Moshi - Kilimanjaro kwenda mkoani Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema Mnamo tarehe 14/03/2015 saa 01:00 asubuhi katika kijiji cha KIDOKA walionekana watu wengi wasiofahamika wakiwa wamejificha katika vichaka na mashamba ya watu.
Sehemu ya Wahamiaji hao wakiwa chini ya ulinzi wa polisi. |
Watu hao walionekana dhaifu, walikuwa wakila mahindi mabichi na wengine wakiomba kwa wanakijiji waliokuwa wakipita maeneo jirani msaada wa chakula na maji ya kunywa kwa ishara, kwa kuwa hawakuwa na uwezo wa kuongea lugha ya Kiingereza wala Kiswahili.
The mdudu, yaani from moshi to dodoma bila ya watu kujua hii ni hatari sn kama taifa..ndugu zangu watanzania kusafirisha watu usiowajua nikosa la jinai so dawa ya hao wasafirishaji watu wasio wajua ni kifungo cha maisha ili iwe fundisho kwa wengine na usarama kwa taifa. ..lakini cha kushangaza kila wanapokamatwa hao madereva wanapewa onyo la mdomo kisha kimiya pasipo na adhabu kali ili waogope lakini onyo la mdomo tupu hata awe nani lazima atafanya tena na tena pasipo na kikomo.
ReplyDeleteKweli hili ni tatizo kubwa sana. Yaani Tanzania kuna baadhi ya watu wana tamaa jamani hata ya kutaka kuuza familia zao. Tuwe na hofu ya Mungu. Tamaa gani hiyo ya pesa? viungo vya albino, ushirikina, uuzaji binadamu, ufisadi, tumo kila aina ya uchafu tumo. Tuone aibu, mataifa mengine yanatuona jamani. Aibu mno mno. Vijana wenyewe maskini hadi huruma jamani. Sina hamu kabisa na tamaa walizonazo watu wachache. Pesa zilimuua Yesu hizo ni laana pesa zikitafutwa bila haki lo!
ReplyDeleteLa! this is just sad. Hawa ni binadamu ati. Treat them nicely jamani.
ReplyDeleteHî vi ni kweli hao ni etiopiska au wasiwasi? Wasiharibie nchi
ReplyDeleteLook at these people! Almost same age group,same sex.same shape,similar faces.It is an indication there is something with this group in Somalia.Whhere are they going,why,what do they leave behind,who takes care of the left families,what is the effect to national economic activities.A lot to be learned,a lot of questions!!!
ReplyDelete