Mshehereshaji wa kongamano la siku moja lililofanyika jijini Dar kuzungumzia ukarabati na uendeshaji wa bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro, Mtaalamu wa masuala ya fedha wa UNCDF, Bw. Imanuel Muro akisherehesha kongamano hilo. Katikati ni mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi akifuatiwa na Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Bw. Peter Malika.(Picha zote na Zainul Mzige)
Na Mwandishi Wetu
ZAIDI ya watu 10,000 wanaozunguka bwawa la Kalemawe wilayani Same mkoani Kilimanjaro watanufaika na ukarabati wa bwawa hilo na kuwekewa muundo mpya wa kiutawala na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Ukuzaji wa Mitaji (UNCDF).
Bwawa hilo ambalo lipo katika kata za Kalemawe na Ndungu lilijengwa na watawala wa Kiingereza mwaka 1952-1959 kwa ajili ya kusaidia shughuli za kilimo na ufugaji baada ya kuanzishwa kwa hifadhi ya Mkomazi na hivyo wakazi kuzuiwa kwenda katika hifadhi hiyo kwa shughuli mbalimbali.
Taarifa ya kuwepo kwa mradi huo mkubwa, imetolewa na Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) nchini, Bw. Peter Malika wakati akiwakaribisha madiwani wa kata hizo ambao wameitwa katika kongamano la siku moja Dar es salaam kuzungumzia ukarabati na uendeshaji wa bwawa hilo.
Pichani juu na chini ni Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Bw. Peter Malika (kulia) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi kufungua rasmi kongamano hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...