Imeripotiwa na Hiroshi Takeuchi Tokyo,Japan, 

Wanamuziki wa kongwe wa muziki wadansi Abbu Omar Njenga aka Abbu Omar na Fresh Jumbe Mkuu wenye ngome yao nchini Japan,siku ya jumamosi 21 Machi 2015 walitia fora kwa kushiriki jukwaani na kumpa baraka zote mwanamuziki Ally Choki katika onyesho lililofanyika katika ukumbi wa Sonudai-Kanagawa Prefecture, Sagamihara City,Tokyo, Japan. 

Wakongwe hao waliobobea katika muziki kwa maiaka mingi Abbu Omar Njenga mpiga gitaa au mpini na mtunzi aliyewahi kutamba na bendi za UDA JAZZ na mwaka 1981 alijiunga na Simba wa Nyika nchini Kenya na hatimaye kujikita nchini Japan kwa miaka mingi na mwenziwe mkongwe Fresh Jumbe Mkuu aliewahi kuwa mwimbaji mtunzi wa bendi za Dar International (Super Bomboka),DDC Mlimani Park "Sikinde na pia Juwata Jazz band aka Msondo Ngoma.
Wakongwe hawa ni mfano wa kuigwa pamoja na kuwa wameliteka soko la muziki wa kiafrika nchini japani na kungineko lakini wapo mstari wa mbele kuwaunga mkono na kuhakikisha kuwa wanamuziki wa nyumbani Tanzania waingiapo Japan wanateka soko. Pia mnaweza kujumuika na mmoja wao at https://www.facebook.com/omar.abbu
Abbu Omar Njenga aka Profesa Abbu Omar na Fresh Jumbe Mkuu kazini
Camarade Ally Choki
Ally Choki na Super Nyamwela
Profesa Abou Omar
Fresh Jumbe Mkuu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...