Na Mwandishi Maalum, New York 
 Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi ambao nchi zao zinachangia wanajeshi au Polisi katika operesheni za kulinda Amani chini ya Umoja wa Mataifa, wanakutana hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa katika mkutano unaoelezwa kuwa wa kihistoria. 
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange na ujumbe wake amewasili jijini New York siku ya Jumatano tayari kuhudhuria na kushiriki mkutano huo ambao utafunguliwa siku ya alhamisi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon . 
 Kwa mujibu wa Waandaji wa Mkutano huu ambao ni Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa, ( DPKO) wameeleza kuwa Zaidi ya Wakuu wa Majeshi 100 watashiriki mkutano huu ambao ni wa kwanza wa aina yake kuwakutanisha Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi kwa wakati mmoja. Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi wanatarajiwa pamoja na mambo mengine, kujadili na kubadilishana mawazo juu ya umuhimu wa operesheni za ulinzi wa Amani katika kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiulinzi na kiusalama yanayoikabili dunia hivi sasa. 
Vile vile wakuu hao watautumia mkutano huu ambao hautakuwa wazi ( closed meeting)kuongeza uelewa na ufahamu juu ya mazingira ya uendeshaji wa operesheni za ulinzi wa Amani , na wanatarajiwa kutoa mchango wa mawazo yao juu ya namna ya kuboresha utendaji na ufanisi wa operesheni za ulinzi wa Amani. 
Katika miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, jumla ya misheni 68 za ulinzi wa Amani zilianzishwa na mpya kabisa ikiwa ni ile iliyoanzishwa ( 2014)katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ( MINUSCA). 
Jumla ya wanajeshi 93,000 na polisi 13,000 kutoka nchi 120 wanahudumu katika misheni 16 ambazo ziko katika mabara manne.Ambako pia kuna raia 17,000 wanaotoa huduma mbalimbali zikiwamo za misaada ya kibinadamu katika misheni hizo. 
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange ameambatana na Brigedia Jeneral MG Luwogo, Brigedia Jenerali HS Kamunde, Lt. Col GM Itang’are na Maj CA Ngh’abi
 Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange akiwa na,  kutoka kushoto,  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na kulia kwake,  Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu,  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  yupo hapa Jijini New York ambako atahudhuria na kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi ambao nchi zao zinatoa wanajeshi au polisi katika operesheni za ulinzi wa amani  chini ya Umoja wa Mataifa
 Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na ujumbe wake  katika picha ya   pamoja na Mabalozi Tuvako  Manongi na  Ramadhan Mwinyi.
Maafisa wa Uwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa wakiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi, pamoja na Mabalozi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...