WAUMINI wa Kikristo waliopata fursa ya kushiriki semina ya
neno la Mungu iliyoandaliwa na mtumishi wa Mungu Mwalimu Christopher Mwakasege
iliyomalizika jana katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam wamesema
wanahamu kubwa na Tamasha la mwaka huu kwa kuwa litakuwa na vitu vya kipekee.
Wakizungumza leo katika viwanja hivyo, walisema
kikubwa ambacho kinaonesha utofauti ni kutimiza miaka 15 tangu kuanza hivyo
kuadhimisha miaka hiyo kutakuwa na mambo tofauti yatakayopatikana siku hiyo.
Waumini hao walisema tamasha hilo ni kubwa hakuna tamasha
lingine kubwa kama hilo ambako watanzania pia wanapata nafasi ya kuwaona
waimbaji wakubwa wa ndani na nje ambao wamekuwa wakiwasikia tu sauti zao.
Walisema kuwa kuna njia tofauti za utoaji wa neno la Mungu
ambako kwa njia ya uimbaji inawashawishi watu wengi hasa vijana kusikiliza
nyimbo na hivyo inakuwa rahisi kumrudia Mungu
hali ambayo inachangia kupungua kwa vitendo viovu.
“Tunalisubiri kwa hamu kubwa Tamasha la mwaka huu maana
linaonekana litakuwa kubwa na tofauti na yaliyopita kwa kweli waaandaji wawe na
moyo huohuo wa kutuletea waimbaji mbalimbali wa kutoka nje tunafurahi kuwaona
na pia tunapata upako mno tunapowaona wanahubili jukwaani” alisema mmoja wa mashabiki hao Debora Kaduma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...