Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma katika Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Joseph J.K. Ndunguru, ambaye anastaafu leo (Ijumaa, Machi 20, 2015) baada ya kutimiza miaka 60, akimlisha keki Katibu Muhtasi wake Bi. Fatuma Ngodoki jijini Dar es Salaam leo huku watumishi wengine wakishuhudia.
Mwanasheria katika Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Charles Mmbando akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma katika hiyo Bw. Joseph J.K. Ndunguru, ambaye anastaafu leo (Ijumaa, Machi 20, 2015) baada ya kutimiza miaka 60.
Mhasibu katika Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Job Kiwory akimiminia kinywaji kisicho na kilevi Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma katika Wizara hiyo Bw. Joseph J.K. Ndunguru, ambaye anastaafu leo (Ijumaa, Machi 20, 2015) baada ya kutimiza miaka 60. Kulia ni Mwanasheria katika Wizara hiyo Bw. Charles Mmbando.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma katika Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Joseph J.K. Ndunguru (mwenye tai) katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria jijini Dar es Salaam leo (Machi 20, 2015). Bw. Ndunguru anastaafu utumishi wa umma leo baada ya kutimiza miaka 60. (Picha: Wizara ya Katiba na Sheria)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Joseph JK Ndunguru aka Mullah utakumbukwa kwa utumishi uliotukuka na uvumilivu usio kifani. Ulilitumikia Taifa pasipo kuchoka mpaka dakika ya mwisho ya kustaafu kwako. Umetuachia alama ambazo ni za kufuatwa kwa watumishi wengine. Nakutakia maisha mema ya kustaafu na milango iache wazi tuchote hekima zako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...