Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Nachingwea, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akimkabidhi kadi ya pikipiki
Mwenyekiti wa Makatibu Kata wa CCM Wilaya ya Nachingwea, Ally Napepa.
Waziri Chikawe alikabidhi pikipiki 35 kwa makatibu kata wilayani humo kwa ajili
kazi ya uendeshaji wa shughuli za chama ikiwemo kuwahamasisha wananchi katika
kata zao kujiandisha ili kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekwa na Bunge,
pamoja na kujiandaa na uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za CCM wilayani humo. Kulia ni Katibu
wa CCM wilaya hiyo, Mussa Liliyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Nachingwea, Mathias Chikawe (kulia) akiwasisitiza Makatibu Kata wa CCM Wilaya
ya Nachingwea, kuzitumia kwa uangalifu pikipiki 35 alizowakabidhi kwa ajili ya kazi
za uendeshaji wa shughuli za chama ikiwemo kuwahamasisha wananchi katika kata
zao kujiandisha ili kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekwa na Bunge, pamoja na
kujiandaa na uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Makabidhiano
hayo yalifanyika katika ofisi za CCM wilayani humo. Picha zote na Felix Mwagara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...