Mhe. Bernard Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Julius James Shirima, mshindi wa Tuzo ya Vijana wa Nchi za Jumuiya ya Madola upande wa Afrika. Kwenye mazungumzo mafupi, Mhe. Membe alimpongeza Shirima kwa tuzo hizo na aliahidi kumpa ushirikiano kupitia Wizara anayoiongoza ili vijana wengi wa Kitanzania wanufaike na mchango wa Shirima na pia waige mfano wake na kuendelea kupeperusha vema bendera ya Tanzania.
Julius Shirima, mshindi wa Tuzo za Vijana wa nchi za Jumuiya ya Madola akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Bernard Membe, ambaye alifanya naye mazungumzo mara baada ya kumaliza kuendesha kikao cha Mawaziri wa Kikosi Kazi cha Jumuiya ya Madola mjini London hivi karibuni. Wengine kwenye picha ni Mhe. Peter Kallaghe, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Bernard Membe, Julius Shirima, Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Balozi Celestine Mushy Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...