Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Bibi wa Kijapan, Midori Uno,machi 17, 2015 kwenye hoteli ya New Otani jijini New York , ambaye aliishi Tanzania miaka ya 60 baada ya Uhuru wa Tanganyika akifanya kazi kwa kujitolea. Hisasa Bibi Uno ni bingwa wa lugha ya kiswahili na amekwishaandika Kamusi ya Kijapan na Kiswahili pamoja na vitabu kadhaa.
Waziri mkuu, Mizengo Pinda na mkewe wakitia saini kitabu cha wageni kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Tokyo nchini Japan baada ya kuwasili ubalozini hapo kuzungumza na Watanzania waishio Japan Machi 17, 2015. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Japan aliyemaliza muda wake, Salome Sijaona na Wapili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Abood Mohamed. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Batilda Buriani na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Mahadh Maalim.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania waishio nchini Japan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wiki kadhaa tuliona mahojiano ya aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Marekani, ndugu Mustafa Nyang'anyi akisema kuwa mabalozi hawakutani kwenye vituo vya kazi. Lazima balozi wa zamani aondoke kwanza ndio mpya aje. Sasa hapo mbona tunamwona balozi wa zamani na mpya wapo kituo kimoja? Ni swali la kiplomasia tu. Naombeni ufafanuzi.

    Mwanafunzi Chuo cha Diplomasia, Kurasini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...