Na Geofrey Tengeneza – Berlin Ujerumani 
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu amekutana na waziri mwenzake wa Biashara na Utalii wa Kenya Bibi Phylis Kandie katika banda la Kenya na kuwa na mazungumzo yanayohusu ushirikiano wa nchi mbili katika sekta ya Utalii. 
Mazungumzo hayo hayakuwa rasmi hivyo hayakuhudhuriwa na wandishi wa habari Aidha Wiziri Nyalandu alitembelea banda la Tanzania na kuzungumza na washiriki wa maonesho ya ITB kutoka makampuni mbalimbali washiriki hao kwa ambapo amewapongeza kwa kuitangaza vema Tanzania katika maonesho hayo.
Mh. Waziri  Nyalandu akihojiwa katika banda la Tanzania na mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha Check inn cha Qatar Bw. Tajamul Hussain kuhusu utalii wa Tanzania kwa ujumla.
MKurugenzi wa kampuni ya usafirishaji watalii ya Zara tours kutoka Moshi Tanzania bibi Zainabu akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalndu alipotembelea banda la Tanzania kujionea namna waoneshaji wa Tanzania wanavyoitangaza Tanzania katika maonesho ya ITB berlin.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akiwa na Waziri wa Biashara na Utalii wa Kenya Bibi Phylis Kandie mara baada ya mazungumzo yao.
Waziri wa Biashara na Utalii wa Kenya Mh. Phylis Kandie akisakata rhumba na Waziri wa Maliasili na utalii wa Tanzania Mh. Nyalandu katika banda la Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...