Wakazi wa eneo la Kwa Mangi kata ya Kibosho Kati wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia,Kinana aliwaeleza wananchi hao kuwa kuna baadhi ya watu wanaotaka nafasi za Uongozi wamekuwa wakijipitisha pitisha kuomba uongozi,hivyo amewaonya na kuwatahadharisha kutojipitisha pitisha kugombea nafasi za uongozi kabla ya muda kuisha na kutangazwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kwa Mangi kata ya Kibosho Kati ambapo aliwaambia wananchi waache kujipitisha pitisha kugombea nafasi za uongozi kabla ya muda kuisha na kutangazwa.
Baadhi ya Kadi zaidi ya 335 za wanachama walizozikabidhi kwa Ndugu Kinana na wamejiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki uvunaji wa mpunga kwenye skimu ya umwagiliaji ya Lower Moshi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda mti wa kumbukumbu kwenye chuo cha Ufundi KVTC,Kibosho wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.
Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Ndugu Cyril Chami akihutubia wananchi wa kijiji cha Chekereni kata ya Mabogeni. Kata ya Mabogeni ina vijiji 8 na vyote vimeshinda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Jimbo la Moshi Vijijini lina Kata 16 ,shule za sekondari zilizojengwa ni 29.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Chekereni kata ya Mabogini.
PICHA NA MICHUZI JR-MOSHI VIJIJINI
Mimi kawaida huwa namfagilia sana Mh Kinana ila leo inabidi niulize, hizo kadi mbona kama zote ni mpya??
ReplyDeleteChe