Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji
cha Misisi kata ya Misisi,wilayani Bahi mapema leo,mkoani Dodoma akiwa
ziarani ndani ya jimbo la Bahi.
Ndugu
Kinana amezungumza na wananchi hao waliokuwa wamebeba mabango na kuzuia
msafara wake,kutokana na matatizo yaliyokuwapo katika kijiji hicho na
kukosa ufumbuzi kwa muda mrefu.Wananchi hao walikuwa na lalamiko lao
moja kubwa lililohusu shule yao ya msingi ya Msisi,ambayo madarasa yake
mawili yaliezuliwa paa (kama yaonekanavyo pichani) na mengine kubomoka
kabisa kufuatia mvua kubwa ilionyesha na kusababisha madhara hayo.
Shule
hiyo ya msingi Msisi ilipatwa na dhahma hiyo mnamo mwaka 2011,na mpaka
leo haikuwahi kufanyiwa ukarabati wa aina yoyote huku walimu na
wanafunzi wakipigwa na jua wakati wa masomo.Ndugu Kinana baada ya
kusikiliza lalamiko hilo kutoka kwa wanakijiji hao,alianzisha harambee
ya papo kwa papo iliyohusu viongozi wa CCM mkoa na Wilaya waliokuwa
kwenye msafara huo na kuichangia shule hiyo na kufanikiwa kupata fedha
na vifaa vya ujenzi ambavyo vitapelekea kuanza upya kwa ujenzi wa madarasa hayo,Aidha Wananchi wa kijiji hicho walimshukuru Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Kinana kwa harambee alioifanya na kupelekea kupatikana kwa misaada
hiyo.
Ndugu
Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wapo kwenye ziara
ya siku tisa mkoani Dodoma ya kukagua,kuhimiza na kutekeleza Ilani ya
Uchaguzi ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza matatizo ya wananchi na
kuyatafutia ufumbuzi.Kinana leo amemaliza ziara yake ndani ya jimbo la Bahi kesho kuunguruma kondoa.
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Msisi akiwa amebeba bango lake kichwani.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akisoma moja ya bango lililokuwa
limebebwa na mmoja wa wananchi wa kijiji cha Msisi,Wilaya ya Bahi
lililohusu shule ya msingi ya kijiji hicho kukosa madarasa ya kusomea wanafunzi,kufuatia mvua mkubwa kuezua mapaa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh Chiku Galawa
na Mbunge wa Jimbo la Bahi,Mh Omari Badwel wakishiriki uchimbaji wa
mitaro na kufukia bomba za maji,katika kijiji cha Nguji kata ya Mundemu
wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.Mradi huo wa maji unatarajiwa kuhudumia
zaidi ya watu elfu tatu,aidha mradi huo uliogharimu kiasi cha fedha
zaidi ya Milioni mia saba unatarajiwa kukamilika Aprili 15,2015.
Wanachi
wa kijii cha Chonde wakishangilia wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana alipokabidhiwa Mkuki na kuvalishwa mgolole ikiwa ni ishara ya
kuwa mmoja wa wazee wa kijiji hicho cha Chonde.
Baadhi
ya wananchi wa kijiji cha Chonde wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana alipowahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara,wilayani
Bahi mkoa wa Dodoma.
PICHA NA MICHUZI JR-BAHI
HABARI PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
PICHA NA MICHUZI JR-BAHI
HABARI PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
MH. ABDULLAHAMAN KINANA, NDIYE ANAYE STAHILI KUWA RAIS WA TANZANIA AWAMU INYOFUATA, NI MCHAPAKAZI WA KUTISHA NA NDO ANAYE IFANYA C.C.M IWE HAI.VERY GOOD I LOVE HIM.
ReplyDelete