Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukielekea katika kijiji cha Gonjanza kata ya Suji,kuzindua mradi wa masi safi na salama sambamba na kuzungumza na wananchi,wilaya ya Same Magharibi mkoani Kilimanjaro.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpungia mkono mkazi wa kijiji cha Gonjanza kata ya Suji,Msafara wa Kinana ulikuwa ukielekea katika hicho kuzindua mradi wa masi safi na salama sambamba na kuzungumza na wananchi,wilaya ya Same Magharibi mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi ikiwa pamoja na kukagua,kusimamia na kuhimiza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.

 
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk.David Mathayo David wakinywa maji ya bomba mara baada ya Katibu Mkuu kuzindua mradi wa maji safi na salama kwa wananchi wa kijiji cha Gonjanza kata ya Suji
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Gonjanza kata ya Suji
 wakazi wa kijiji cha Gonjanza kata ya Suji wakifurahia kupatikana kwa maji katika kijiji hicho,ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk.David Mathayo David walizindua mradi huo 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijibu baadhi ya changamoto za wananchi wa Hedaru waliomsomea kwenye risala yao, Katibu Mkuu alipita Hedaru kushiriki na kukagua ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Hedaru.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk. David Mathayo David wakati wa mapokezi katika kata ya Njoro .Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi ikiwa pamoja na kukagua,kusimamia na kuhimiza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa kata ya Njoro ikiwa ni kituo cha kwanza katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM jimbo la Same Magharibi.

PICHA NA MICHUZI JR-SAME MAGHARIBI 

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...