Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (wa pili kulia)akishiriki ujenzi wa tanki la maji katika Kijiji cha Sakala, wilayani Ngorongoro.Ndugu Kinana na ujumbe wake wako kati wa ziara ya siku tisa mkoani Arusha ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Komredi Kinana akisaidiana na Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, Telele kujenga vyumba vya madarasa ya kidato cha nne na cha tano katika Shule ya Sekondari Samunge, wilayani Ngorongoro.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM kijiji cha Wasso Ndugu Revocatus William Parapara. Awali ndugu Revocatus William Parapara alikuwa Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Ngorongoro kwa takribani miaka 15.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhi mbuzi kutoka kwa baraza la Wafugaji kwa Wananchi wasiojiweza ili kupambana na baa la njaa linalowanyemelea.Kila kaya ilikabidhiwa mbuzi 15,ambapo idadi ya mbuzi wapatao 2470 walikabidhiwa kwa wananchi hao na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana.
Komredi Kinana akigawa mbuzi bure kwa wajane kila kaya mbuzi 15 zilizotolewa na Baraza la Wafugaji Ngorongoro kwa kushirikiana na Hifadhi ya Ngorongoro ili kuwapunguzia watu hao umasikini.

Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
akigawa mbuzi bure kwa wajane kila kaya mbuzi 15 zilizotolewa na Baraza la Wafugaji Ngorongoro kwa kushirikiana na Hifadhi ya Ngorongoro ili kuwapunguzia watu hao umasikini.

Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wanakijiji cha Naoinokanoka,Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha mapema leo,Kinana pamoja na kuwahutubia wananchi hao pia aliruhusua kuulizwa maswali mbalimbali likiwemo suala la mipakya ya hifadhi ya Ngorongoro na vijiji vyao,ambapo pia hawaruhusiwi hata kulima zao la aina yoypte kwenye makazi yao

Aidha walieleza kuwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda aliwahi kufanya ziara katika kijiji hicho na kuahidi  kuwa serikali itatoa magunia 10 ya mahindi kwa kila kaya kwa mwaka ili kupunguza makali ya njaa kutokana na ukame,  Jambo ambalo halijatekelezwa mpaka sasa. 

Akijibu hoja zao Ndugu Abdulrahman Kinana amesema hawezi kujibu lolote kwa sasa ili asije kuonekana amedanganya.   lakini ameahidi kurudi kijijini hapo baada ya mwezi mmoja mara baada ya kukutana na Mawaziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi na kupata taarifa juu ya ahadi ya Waziri Mkuu pamoja na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro pamoja na mhifadhi wa Ngorongoro ili kuzungumzia suala hilo kwa ajili ya kupata ufunbuzi wa kudumu.  
 PIchani ni baadhi ya Viongzi wa Baraza la Wafugaji,Viongozi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na wazee wa Kimila wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuhusiana na mambo mbalimbali yahusuyo ardhi
Picha Kati ni Ndugu Kinana akiwa na baadhi ya viongozi wa chama wakishiriki kupaka rangi jengo la nyumba ya mganga katika kijiji cha Bulati,wilayani Ngorongoro.

PICHA NA MICHUZI JR-NGORONGORO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...