Utendaji wa TFDA Katika Udhibiti wa Bidhaa Za Vyakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa Tiba Wapongezwa
Katibu Tawala (RAS) wa Mkoa wa Arusha, Bw. Adon S. Mapunda, akiwakaribisha wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa TFDA (MAB) wakati walipofanya ziara ofisini kwake mapema wiki hii kwa lengo la kujadili mikakati ya kudhibiti  chakula, dawa na vipodozi mkoani Arusha. 
Pamoja na mambo mengine, Bw. Mapunda aliipongeza TFDA kwa utendaji kazi mzuri na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kulinda afya ya jamii.  Kushoto ni Mwenyekiti wa MAB, Balozi Dkt. Ben Moses na anayesaini kitabu cha wageni ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA na Katibu wa MAB, Bw. Hiiti Sillo.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, akisisitiza jambo wakati wa kikao na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha kuhusu utendaji kazi wa TFDA Kanda ya Kaskazini wakati wa ziara ya Wajumbe wa MAB na Menejimenti ya TFDA   Ofisini kwa RAS mapema wiki hii.  Wengine katika picha ni wajumbe wa MAB na Menejimenti ya TFDA.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Bw. Juma Iddi,  akimsikiliza Mwenyekiti wa MAB  Balozi Dkt. Ben Moses (aliye kulia kwake) wakati wajumbe wa Bodi hiyo walipofanya ziara ofisini kwake mapema wiki hii kwa lengo la kujadili mikakati ya kudhibiti  chakula, dawa na vipodozi mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa MAB, Balozi  Dkt. Ben Moses, akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Bodi hiyo wakati wa kikao cha kujadili mikakati mbalimbali ya utendaji  kazi wa TFDA kilichofanyika katika ofisi ya TFDA Kanda ya Kaskazini  Jijini Arusha mapema wiki hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...