Naibu waziri wa Maji Amos Makalla ameendelea na ziara katika mkoa wa Lindi na leo amefanya ziara katika jimbo la Mchinga kwa kutembelea vijiji vya Kitohavi na LIHIMILO ambavyo vina shida ya maji kwa muda mrefu huku serikali ikiwa ameviweka vijiji hivyo katika mpango wa Matokeo ya haraka
Akiongea katika mikutano ya hadhara ameagiza uongozi wa halmashauri ya Lindi kuchimba visima virefu ndani ya wiki mbili kwa kuwa wizara yake ilishatuma fedha za kuchimbia visima hivyo na haoni sabababu za viongozi wa halmashauri hiyo kuendelea kuchelewa kuchimba visima hivyo huku utafiti na usanifu ulishafanyika muda mrefu na bei za kuchimba visima inaeleweka
Mbunge wa jimbo la Mchinga Mhe. Said Mtanda ameishukuru serikali kwa hatua hii muhimu ambavyo itapunguza kero ya Maji katika vijiji vya Kitohavi na LIHIMILO.
![]() |
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akisisitiza Jambo wakati wa mkutano wa hadhara kijiji cha Lihimilo jimbo la Mchinga mkoani Lindi |
![]() |
Mbunge wa jimbo la Mchinga Mhe Said Mtanda akimkaribisha naibu Waziri wa Maji. |
Naibu Waziri akizungumza na wananchi wa kijiji cha LIHIMILO ambapo walikuwa na hamu kubwa ya kusikiliza Kauli yake juju ya suala la kuchimbiwa Kisima.
Maji yachimbwe ndiyo. Lakini na wananchi pia wahamasishwe hata kusaidiwa kujenga nyumba bora. Jinsi huduma za umeme, maji zinavyo endelea kufikia wananchi hivi sasa wanahitaji nyumba bora kama njia ya kuboresha maisha yao na afya zao.
ReplyDelete