Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban  Ki Moon akiwa na  Viongozi wa Madhehebu  mbalimbali ya Dini mara baada ya  viongozi hao wa dini kuzungumza katika mkutano wa ngazi ya juu uliojadili  pamoja na mambo mengi kuongezeka kwa vurugu zitokanazo na itikadi kali za kidini na ukereketwa wa kupindukia na  nini kifanyike kukabiliana na  changamoto hiyo. katika picha hii yupo pia Rais wa Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa, Bw. Sam Kutessa ambaye ndiye aliyandaa mkutano huo.
Na  Mwandishi Maalum, New York
 Kufuatia ongezeko la  makundi ya dini  yenye itikadi , matukio ya  kigaidi,  kukosekana  kuvumiliana na maridhiano,  Katibu Mkuu wa     wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amewageukia viongozi wa  madhebu ya  mbalimbali  dini  duniani akiomba busara zao na uongozi wao.

Amesema, busara na uongozi wa madhehebu  hayo ya dini  unahitajika sana  katika kuhubiri na kueneza kuvumiliana,  maridhiano,  stahimili,  kuheshimiana na kujenga utamaduni wa kuzungumza   miongoni wa  jamii bila ya kujali dini zao au rangi zao.

SOMA ZAIDI HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hili suala la kuharibu kwanza kisha ndio kukimbilia msaada na huruma ya viongozi wa dini hata kwetu lipo sana...juzijuzi tu kuna msemo kutoka ktk kitabu kitukufu kuna mtu alipewa kibusara kwamba ...ukishupaza shingo utavunjika na hutopata dawa....Ukiangalia kwa makini utaona ni visasi tu baada ya watu kuteswa bila sababu, nchi nyingi raia wake wamekimbia kwa sababu ya vita visivyo na kichwa wala miguu......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...