Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde toka Wilayani Rungwe, Jijini Mbeya inaeleza kuwa Basi dogo aina ya Toyota Hiace imetumbukia kwenye Mto Kiwira mapema leo na inadaiwa kuwa zaidi ya watu 20 waliokuwepo kwenye basi hilo wamepoteza Maisha.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, amesema kwamba ajali hii imetokea wakati Mabasi yafanyayo safari zake kati ya Mbeya na Kyela (maarufu kama Coaster) kugoma kutoa huduma ya kusafirisha abiria katika maeneo hayo, hivyo baadhi ya hiace za mjini kuamua kubeba abiria, hali iliyopelekea hiace hizo kubeba abiria wengi zaidi ya uwezo wake.

Inaelezwa kuwa gari hiyo ilipoteza muelekea na kuingia mtoni, baada ya dereva wake kushindwa maarifa kutokana na mwendo aliokuwa nao.

Mungu aziweke pema roho za marehemu hao,Amin.
Pichani ni Baadhi ya wakazi wa maeneo ya jirani na ilipotokea ajali hiyo wakiiangalia basi hiyo ikiwa kando kando ya mto Kiwira.
Wananchi wa Mji wa Kiwira wakienda kuangalia ajali hiyo.
Sehemu ya wananchi wa Mji wa Kiwira wakiangalia Baadhi ya Miili ya Watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. SERIKALI TANGU MUWAACHIE HAWA MADEREVA MBULULA WAENDELEE BILA KUPATA UTAALAM SASA NI VIFO KWENDA MBELE

    ReplyDelete
  2. Tamaa, tamaa, tamaa ya pesa inatuuwa jamani. Okoa maisha ya watanzania kwa kukataa tamaa ya pesa na tutafika. Madereva acheni kukatisha maisha ya watu kila siku, acheni tamaa jamani. Askari wa usalama barabara

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...