Mshinda wa kitita cha shilingi milioni 10/- kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Shamila Ramadhani(kushoto)akikabidhiwa hundi yake na Balozi wa promosheni hiyo Hillary Daud ‘JayMillions’ baada ya kuipuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo katikati ni mume wa mshindi huyo Abdallah Mahoka.Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Dar Live wakati wa Tamasha la Mwana Dar Live lililofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba akiwapagawisha washabiki wa muziki wake waliofurika katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhamini na Vodacom Tanzania, Katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mamaa Aisha Mashauzi akitumbuza muziki wa Taarabu katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhamini na Vodacom Tanzania, Katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
Msanii wa nyimbo za mchiriku Sueleman Jabiri”Msaga Sumu”akisaga sumu ipasavyo kwa washabiki wa muziki wake wakati wa Tamasha la Mwana Dar Live lililodhamini na Vodacom Tanzania, Katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
Hongera dada kwa ushindi huu, ili uendelee kuwa milionea nashauri uwekeze sehemu ya pesa hizo katika mradi utakaoendelea kuzalisha. Usikimbilie tu kuvaa nguo za rangi rangi na mikufu mingi ya dhahabu wekeza pia.
ReplyDeleteHadi wasaga sumu wanaweka swaga na kuvaa kata k.Mbona haviendani na fani ya mchiriku!
ReplyDelete