IMG_1562
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu (wa tatu kushoto) akiwa na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (wa tatu kulia), Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago (kulia), Mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na Mtanzania Chef Issa Kapande (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kuwasili kwenye mnuso wa uzinduzi wa mgahawa huo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi Maalumu, 
Trollhattan-Sweden
MGAHAWA mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani, Issa Kapande `Chef Issa’, umefunguliwa nchini Sweden na kuvunja rekodi ya kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote barani Ulaya unaopicha vyakula vya Kiafrika.
Mgahawa huo ulizinduliwa na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu.
Balozi Msechu alimpongeza  Chef Issa Kapande na mkewe kwa kufanikisha kuwapo kwa mgahawa huo ambao umeweka rekodi kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote ya Kiafrika katika nchi za Ulaya.
Aidha, alimshukuru Torvald Brahm mwenyeji wa mji huo kwa kumuunga mkono Issa hadi kufanikisha ndoto yake ya kuwa na mgahawa wa kwanza wa Kiafrika katika mji wa Trollhattan utakatoa huduma ya chakula cha kitanzania.Katika uzinduzi huo ambapo wenyeji wa manispaa hiyo akiwemo Meya na mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund na msaidizi wake Peter Eriksson walikuwepo, balozi ambaye ndio kwanza ameanza kazi alielezea kufurahishwa na juhudi za Kapande.
IMG_1477
Wadau wakiwa nje ya ukumbi tayari kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa mgahawa huo.
IMG_1567
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akiwa na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (kushoto) pamoja na Chef Issa Kapande (kulia) wakielekea kwenye eneo la tukio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hongera kwa kuthubutu kuwekeza nje ya nchi

    ReplyDelete
  2. give credit where credit is due, safi sana.
    I hope and pray the first day is an indication of what is about to follow

    ReplyDelete
  3. Kila la kheri chef tunamuomba M'Mungu kheri na baraka ktk biashara uliyoanzisha.

    ReplyDelete
  4. ningeomba mrekebishe maelezo ya watu walio kuwemo. Nimetuma maelekezo

    ReplyDelete
  5. Hongera mkuu kwa uwekezaji mkuu.

    ReplyDelete
  6. Hongera sana. Hii inajustify kuishi nje ya nchi. Naona Afisa wa Mambo ya Nje Bwana Adam Isara nae alikuwepo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...