Timu ya Tanzania, FC Kilimanjaro ambayo ni mabingwa wa soka la Afrika nchini Sweden imepata ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya watani wao wa jadi Kenya kwenye mechi maalum ya kirafiki ya Amani na Upendo iliyofanyika jijini Stockholm jana tarehe 11 Aprili, 2015
Mechi hiyo iliandaliwa kwa pamoja na Balozi za Kenya na Tanzania nchini Sweden kwa kushirikiana na wanadiaspora wa nchi hizo kwa madhumuni ya kuonyesha mshikamano na kuziombea nchi zetu amani na upendo kufuatia matukio ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni nchini Kenya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...