Innalillahi wa Inna Ilaihi Rajioun:SUPREME Mufti wa Uganda ambaye pia ni Murshid wa Twariqatus-Shaadhuliy nchini Uganda, Sidi. Sheikh Zubeir Kayongo amefariki dunia katika hospitali ya Agha Khan Jijini , Dar es salaam jana alikokuwa amelazwa muda mfupi akiwa njiani kuelekeya Kilwa Pande kuhudhuria HAUL na Ziyarah ya kutimiza miaka 100 ya Sidi.Sheikh Muhammad Al- Maaruf As-Shadhuly(QAS).
Marehemu aliwahi kuhudhuria Ziyarah ya Mawlid Jijini Unguja Mfunguo 6. na Twariqatul Shaadhuliya nchini humo ilimfanyiya hadhra maalum kwa heshima yake katika Msikiti wa Mwembetanga Jijini Unguja.Ilikuwa ni desturi ya .Al-Marhum SUPREME Mufti wa Uganda kila mwaka kuhudhuria Hawl ya Sheikhe Muhammad Al Maarufu aliyeleta Twariqatu Shadhuliyah Afrika ya Masharika mwanzoni mwa miaka ya 1900 toka huko Akka Palestina inayokaliwa kwa Mabavu alipochukua Twariqah hiyo toka kwa Sheikhe lake Sidi Sheikh.
Ali Nurdin Al-Yashurutwi(QAS).Twariqah ya Shadhuli imeenea maeneo mengi duniani ikiwemo Uganda ambapo ilifika miaka ya mwanzoni mwa 1900 chini ya Sidi.Sheikh.Hussein Ibn Hussein wa Kilwa Pande aliyepokea Twariqah toka kwa Sidi Sheikh Muhammad Al-Maarufu wa Ngazija.
Nchi zingine zilizoenea Twariqah hii ni Misr, Morocco(Maghreb), Algeria,Tunisia, Sudan, Sri-Lanka, India, Pakistani, Jerusalem(Palestina),Libya, Uingereza, America, Canada, Australia, Afrika Mashariki na mwanzilishi wa Twariqah hii akitokea huko Morocco na aliyetawafu huko nchini Misri akielekea safari ya Hajj kwa umaarufu akiitwa Sidi.

Sheikh Abal Hassan As-Shadhuly, Jina la Shadhuly linatokana na mji wa huko Afriqiyah(Tunis) ambako ndipo harakati za Sheikhe zilipoanzia kueneza Daawah ya Kitwariqah yenye kushikamana na Quraan na Sunnah kwa mujibu wa mafundisho ya Ahlul Sunnah walJamaa..
Watu wengine maarufu waliokuwa wakifuata Twariqah hii ni Imam alHafidh Jalaludin As-Suyutwi aliyekuwa mufasir maaruf wa Quraan na Hadith (Tafsir Jalalayn),Sidi Sheikh Umar Mukhtar As-Sanusi(mwanaharakati wa Ki-Libya maarufu kama The Lion of The Desert), Shahidi.Sidi.Sheikh Hassan Al-Bannah(Rahimahullah) mwanzilishi wa harakati Ikhwaan Al- Muslimun ya nchini Misri, aliyekuwa Mfalme wa Libya Mfalme Idriss aliyepinduliwa na Kanali Muammar Gadafi Wengine katika karne ya sasa ni wanachuoni wakubwa wa Hadith huko Maghreb wajulikanao kama Saadah al-Ghumari ,, Mwanachuoni wa Hadith wa Alexandria Al-Kahtan, pia aliekuwa Mufti wa nchi ya Misr, Sidi.Sheikh Dr.Ali Gumua na Maulamaa wengine wengi wa Al-Azhari Shariyf na Qarawiyin University huko Maghreb ni Murshid wa Twariqah hii ya Shadhuly..Tunamuomba Mola Amjaalie Mayiti wetu Sheikhe letu Sidi.Sheikh Zuberi Kayongo msamaha wa mapungufu yake na Amjaalie Mayiti wetu pepo iliyo juu kabisa na tunamuomba Mola amtakase mayiti wetu kama inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na madhambi yake na amjaalie kaburi lake liwe ni katika viwanja vya pepo , Tunamuomba Mola wetu ampe majazo mema kutokamana na amali zinazoendelea na zile zitakazofanywa kwa niaba yake iwe na mimea au viumbe katika wanadamu,Malaika na Majini Yaa Raab.
Inna lillahi wa Inna ilayhi rrajiuun.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu ampe makazi mema peponi apokewe kwa furaha na amani.
Aaamin