Mkongwe kwenye Muzuki wa Kizazi Kipya Nchini Tanzania Juma Khassim Kiroboto Maarufu kama Juma Nature @Sir_Nature amesema Kuwa Siku za Karibuni Zijazo atamuoa Mpenzi wake Ambaye anatokea Arusha.
Akifanya Mahojiano na @DjHaazu wa @MamboJamboRadio Arusha Tanzania, Juma Nature amesema kuwa amekaa bila Mke wa ndoa kwa kipindi Kirefu sana tangua aachane na alikuwa Mkewe ambaye Alibahatika Kuzaa Mtoto mmoja na yeye aitwaye FURAHA na kwa sasa anaamini ni Muda Muafaka wakufikia Hatua Nyingine ya Kuitwa Baba wa Familia.
Katika Mazungumzo hayo @Sir_Nature amesema pia kwamba Mwanaye Furaha anaishi na mama yake ila yeye kama Baba anamgharamia mwanaye Kila kitu ikiwa ni Pamoja na Shule Bora huku akisema kuwa yeye na Mzazi mwenzake huyo hawana Shida wako Sawa japo Mzazi mwenzake huyo alipata Bwana Mwingine na Kuolewa.
Katika Point nyingine Pia Nature amewaomba Mashabiki wake wakae Tayari kwani Karibuni anaachia Wimbo wake Mpya wenye Mahadhi ya Kwaito aliosema utaitwa GUSA UNASE.

MSIKILIZE  JUMA NATURE AKIONGEA NA @DjHaazu KWA KU-CLICK LINK HII ----> JUMA NATURE - AKIZUNGUMZA NA DJHAAZU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. UNAWAPENZI WANGAPI NA HIVI UMEAMUA KUMUOA YULE WA ARUSHA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...