
Habari zilizotujia hivi punde zinasema Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), amefariki dunia asubuhi hii katika hospitali kuu ya Jeshi, Lugalo, jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa za kifamilia, mazishi yanatarajiwa kufanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam siku itayotajwa kesho na sio Jumanne kama ilivyotangazwa awali.
Msiba upo nyumbani kwa marehemu Chang'ombe jirani na TCC Club jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa za kifamilia, mazishi yanatarajiwa kufanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam siku itayotajwa kesho na sio Jumanne kama ilivyotangazwa awali.
Msiba upo nyumbani kwa marehemu Chang'ombe jirani na TCC Club jijini Dar es salaam.
Mzee Mbita atakumbukwa Tanzania, bara zima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni barani Afrika, hususan utawala kidhalimu wa makaburu Zimbabwe na Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa Nelson Mandela.
Mjane wa marehemu Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita, Ngeme Mbita (katikati) akiwa na waombolezaji wengine nyumbani kwa marehemu, Chang’ombe jijini Dar es Salaam leo. Brigedia Mbita amefariki leo katika Hospitali ya Lugalo. (Picha na Francis Dande).
Roho yake ipumzike katika Amani ya Milele mikononi mwa Mwenyezi Mungu, Amina.
ReplyDeleteMay his soul rest in eternal peace! General Mbita was a true son of Africa.
ReplyDeleteInnaa lillaahi wainnaa ilayhi raajiun.Allah amsamehe makosa yake na amuingize peponi.ajaalie azikwe kesho,asiekwe sana kama inavyoanza kuzoeleka.amin
ReplyDeleteMay he rest in peace. It's a pity that he has gone while witnessing the current Xenophobia in South Africa as a "Thank You Note" For His Sweat in the South Liberation Struggle. I know that Mugabe is in mourning.
ReplyDeleteMay your soul rest in eternal peace.
ReplyDeleteMungu ampumizishe mahali pema. Ila ukombozi wake ulikuwa hauna maana manake tunaona sasa Afrika ya Kusini inavyowabagua afrika wenzio.
ReplyDeleteInna Lillah Waynna Illahy Rajioun.
ReplyDeleteInna Lillah.......
ReplyDeleteMungu amfungulie pepo kwa kazi alizofanya na misaada aliyowapa binAdam wenzake hapa duniani.He was an achiever and I remember him from Tabora Boys
God give peace of mind to his family and friends.
Ibrahim Manthy.
Poleni sana wafiwa Mungu awatie nguvu wakati huu wa msiba. Huyu mzee wa changombe uhindini/TCC tumekaa naye vizuri yeye na jamii yake siku nyingi.
ReplyDelete