Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, HASSAN MTENGA akijibu maswali ya wananchi wa tarafa ya pawaga.

Na Fredy Mgunda,Iringa

Katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Iringa, Hassani Mtenga amewataka wananchi wa tarafa ya Pawaga katika jimbo la Isimani kuendelea kumwamini Mbunge wa jimbo hilo kwa kuwa anawatendea haki kwa kuwaletea maendeleo.

akizungumza katika mkutano huo, MTENGA amewataka wananchi kuendelea kukiamini chama hicho kutokana na kutekeza ahadi zao ambazo wanakuwa wanaziahidi kwa wananchi.

Kwa upande wao wananchi kijiji cha boliboli kilichopo tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa Vijijini wanakabiriwa na matatizo ya kiafya pamoja na migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na wakulima hayo yamebaini katika mkutano ulifanyika katika kijiji hicho.

katibu wa CCM mkoa wa iringa HASSAN MTENGA
akiwapa vifaa vya michezo wananchi wa
 tarafa ya pawaga
wakizungunza wakati wa mkutano huo wananchi hao wamesema kuwa kijiji hicho hakina mganga wa kutoa huduma katika zahanati yao na kuongeza kuwa tatizo la migogolo ya aridhi limekuwa kubwa.

Akijibu maswali ya wananchi hao katibu wa ccm mkoa wa iringa hassani mtenga amewata viongozi wa chama hicho kufanya mikutano ya mara kwa mara na kupokea kero za wananchi na kuzitatua mapema ili kuendelea kukijengea imani chama chao.

Viongozi wengi wamekuwa hawawajali wananchi wao ambao wamewaweka matarakani na ndio imekuwa sababu ya matatizo mengi na migogolo mikubwa katika vijijini.

Lakini MTENGA amesema swala mfureji,tatizo la mganga,walimu kuwa walevi na mgogoro wa mbomipa anayachukua na kwenda kuyafanyia kazi na kuwaahidi kuwa matatizo yote waliomweleza yatatulika.

“Alimalizia kwa kuwaomba wananchi kuipigia kura katiba inayopendekezwa ili waweze kupata katiba ya wananchi na kuwaambia wananchi wa eneo hilo kuitumia fursa ya kuijiandikisha katika daftari la kudumu la kupigia kura ambalo iringa litaanza tarehe 29 mwezi huu” alisema HASSAN MTENGA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...