Kijana Amosi Peter Rwangarya ambaye ni mtanzania mwanafunzi nchini Serbia akiwa anawakaribisha wanafunzi wa Kiserbia (Ulaya Mashariki) kujifunza Kiswahili kwenye ukumbi wa African Museum jijini Belgrade (Serbia).
Amosi Peter Rwangarya(kulia) na Galina Tudyk (kushoto) ambaye ni Mserbia aliye wahi kukaa East Afrika kama Kenya na Tanzania na anaongea kiswahili na ni mwalimu wa lugha mbalimbali haswa kiingereza na Kiserbia na hapo mbele ni wanafunzi wanaojifunza kiswahili nchini humo.
Amosi Peter Rwangarya ni mwanafunzi wa Kitanzania nchini  Serbia kwa scholarship ya serikari hizi mbili. Amekuwa nchini Serbia sasa kwa takribani miaka minne akichukua shahada yake  ya kwanza ya uchumi, ambapo katika hii scholarship kuna wanafunzi kutoka nchi takribani 50  za dunia hasa za kiafrika. 
Yeye amekuwa mmoja ya Watanzania kuchagulia na African Museum nchini humo kufundisha lugha ya kiswahili kwa beginners wa ikiwa ni pamoja na utamaduni wa Waafrika kutambulika duniani na kuwezesha utalii hasa Afrika Mashariki kuwa rahisi kwa watu hao wa Ulaya Mashariki wajapo kutalii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamani nafurahi kusikia, mimi niko sweden na ni mwalimu wa kiswahili. Nimekosa kabisa mwenzangu hapa anayefundisha kiswahili na inakuwa ngumu kwangu kupata materials. Kama kuna mtu tuwasiliane kwa email linda.johansson5@kungsbacka.se

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...