MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad leo amehudhuria katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba na wenzake 30 wa chama hicho.

Maalimu Seif alifika na msafara wake wa magari matatu Mahakamani hapo  majira ya saa nne asubuhi.

Hakimu wa Makakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Cyprian Mkeha amesema washitakiwa hao wanadaiwa kufanya kosa la jinai la kufanya mkusanyiko usio halali kwa mujibu wa sheria za nchi.

Hakimu huyo ametoa dhamana kwa watu wote kutokana na maelezo yao kama masharti ya dhamana yalivyokuwa yakihitajika 

Hakimu huyo, amesema kuwa  kesi inayomkabili Profesa Lipumba na wenzake 30 ni ya kufanya mkusanyiko usio halali kwa mujibu wa sharia za nchi mnamo januari 22 na 27 maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam na upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika.

Jopo la mawakili wa kesi hiyo likiongozwa na Wakili,Job Karario awali walipeleka pingamizi la mashtaka dhidi ya Profesa Lipumba na wenzake 30.

Hakimu  Cyprian aliahirisha kesi hiyo mpaka itakapotajwa tena Mei 6 mwaka huu na washitakiwa wote katika kesi hiyo wamepewa dhamana.

 Akizungumza baada ya kutoka Mahakamani hapo ,Maalimu Seif Sharif Hamad amesema anashukuru wanachama kwa kujitokeza kwa wingi pamoja na kuwatolea washitakiwa dhamana.

Amesema wanachama waendelee kuwa na moyo wa kujitoa katika matatizo kwani wote wako katika safari moja katika chama.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF)Profesa Ibrahim Lipumba akiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini Dar es Salaam kwa kutuhumiwa kufanya kukosa la jinai kwa kushawishi wafuasi wa cha hicho kufanya mkusanyiko usio halali.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Maalim Seif Shariff Hamad (mwenye suti ya kijivu)akiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini Dar es Salaam, akisikiliza kesi inayomkabili wa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Liipumba na wenzake 30 wakituhumiwa kufanya mkusanyanyiko usio halali. (Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...