Na Hassan Hamad, OMKR
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameweka mawe ya msingi na kupandisha bendera katika matawi na barza sita za CUF ndani ya Jimbo Kitope Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja.
Matawi na barza alizoweka mawe ya msingi ni pamoja na Kiombamvua, Mkaratini, Mgambo, Kilombero, Kipandoni na Kiwengwa Cairo.
Hata hivyo, mkutano wa hadhara uliokuwa ufanyike katika viwanja vya Kipandoni umehairishwa, kwa madai kuwa haukupata kibali kutoka kwa jeshi la polisi.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika barza ya CUF ya WENYE WIVU WAJINYONGE katika eneo la Kitope Mkaratini.
.Vijana wa barza ya HATUDANGANYIKI ya Kiwengwa Cairo wakimsikiliza Maalim Seif wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika barza hiyo (Picha na OMKR)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...