Na  Bashir  Yakub.
Suala   la  matunzo  haliishi  tu kwa  mtoto/ watoto.  Wengi  wa  wanaume wamekuwa  wakipendelea  kuwajibika  kwa  kutoa  matunzo  ya  watoto  na  kumuacha  mwanamke.  Jambo  hili  si  sawa  na  halikubaliki  kisheria. Ni  vema  kufahamu    kuwa  suala  la matunzo  kwa  mwanamke  limegawanyika   mara  nne.  Kwanza   kuna  matunzo  kipindi  ambacho  ni  cha  ndoa  ambapo  hakuna  mgogoro  wowote  baina  ya  wanandoa. Pili  kuna  matunzo  kwa  mwanamke  kipindi  ambacho  wanandoa  wanakuwa  wametengana  lakini  hawajatalikiana.  Tatu   kuna  matunzo  kwa  mwanamke   kipindi   ambacho   kuna mgogoro  wa  familia mahakamani,  na   nne  matunzo  kwa  mwanamke  kipindi  ambacho  talaka  imekwishatolewa.
1.MATUNZO  YA  MWANAMKE   WAKATI  WA  NDOA.
Hiki  ni  kipindi  ambacho   ndoa  huwa  inaendelea   vyema  bila  kuwapo  kwa  mgogoro  wa  aina  yoyote  ambao  unaweza  kutishia  uwepo  wa ndoa  hiyo.  Katika  kipindi  hiki   mwanaume ana  wajibu  wa  kisheria  kutoa  matunzo  kwa  mke  wake. Hii  ni  kwa    ndoa  zote   yaani  zile  za  kimila, kiserikali,  kidini  ikiwemo  ile  ya  kuishi  wote  kwa  zaidi  ya  miaka  miwili ( presumed  marriage). Mwanaume  yeyote  ambaye  anaishi  na  mwanamke  katika  ndoa  mojawapo  kati  ya  hizi  basi  huyo  anawajibika   kutoa  matunzo  kwa    mwenza  wake.
2.MATUNZO   KWA  MWANAMKE   KIPINDI  AMBACHO  AMETENGANA  NA MME  WAKE.
Kisheria   kuna  tofauti  kubwa  kati  ya  kutengana  na  kutalikiana.  Kutengana  ni  kutengana  na  inaweza  kuwa  waliotengana   wanaishi  nyumba  moja  lakini  vyumba tofauti  au   vitanda  tofauti.  Lakini  pia  inawezekana  waliotengana  wakawa  wanaishi  nyumba  tofauti  na  sehemu  mbali  kabisa.  Huku  kote ni  kutengana  wala  sio  kutalakiana au  kuachana. Kwa  hiyo  wanaume walio  katika  kipindi  cha  kutengana  na  wake  zao   wanawajibika  kutoa  matunzo  kwa  wanawake  hao.  Hii  ni  kwa  mujibu  wa  sheria  wala  si  vinginevyo.  Haki  ya  mwanamke  kutunzwa  inabaki  palepale  japo  hukai  nae  chumba  kimoja,  hauli  chakula  chake, haukai nae  nyumba  moja, na  wala  hamshirikiana   chochote.  Hii  ina  maana  kuwa  kutoshirikiana  naye  katika  haki    yoyote  ya  ndoa hakuondoi  wajibu  wa  kisheria  wa   kutoa  matunzo  kwa  mwanamke  huyo.  Katika  kipindi  hiki  cha  kutengana ni  makosa  kukataa  kumtolea  matunzo  mwanamke. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hii sheria imepitwa na wakati, kwanini mwanamke atunzwe kwani hawezi kujitunza ? , you can`t have both ways, wanataka na wamepewa equal opportunities, halafu tena tuwatunze kwani wao watoto, wazee au hawajiwezi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...