Na Bashir Yakub.
Kumekuwa na tabia ya taasisi za fedha kuuza nyumba au viwanja vya watu walivyoweka rehani na kushindwa kulipa mkopo kwa bei ya kutupa. Kwakuwa taasisi za fedha huamini kwamba wana deni na mtu na ameshindwa kulipa hela zao na pengine kwakuwa tayari wamekamilisha taratibu zote za kisheria za kuuza basi huamua kuuza mali ya mtu kwa bei ambayo ni ndogo kiasi cha kustaajabisha.
Ni kawaida kukuta nyumba ya milioni mia ikiuzwa hata milioni kumi na tano ili kulipia deni la milioni kumi na mbili au kumi na tano. Watu wanapaswa kuelewa kuwa hili si sawa na sheria imekataza jambo hili. Thamani ya nyumba au kiwanja iko palepale hata kama mtu ameshindwa kulipa mkopo. Si kweli kuwa kwakuwa sheria imeruhusu kuuza mali ya mtu anaposhindwa kulipa mkopo basi imeruhusu kuuza bei yoyote ile ilimradi muuzaji amepata kiasi anachodai. Hili si kweli kama tutakavyoona hapa chini.
1.WAJIBU WA TAASISI YA FEDHA KATIKA KUUZA NYUMBA YA DHAMANA. .
Kwa kujua hili la kuuza mali za watu bei ya kutupa Sheria ya ardhi kifungu cha 133 ( 1 ) kikasema kuwa muuzaji wa nyumba iliyowekwa rehani ana wajibu mkubwa na wa hali ya juu kuhakikisha anachukua tahadhari na anakuwa mwangalifu kwa kiwango cha juu kuhakikisha wakati anapouza ardhi ya mtu anaiuza kwa bei nzuri na bei ambayo inakubalika kuwa bei inayostahili kwa wakati husika.
Huu ni wajibu wa kisheria alionao muuzaji au mnadishaji wa ardhi ya dhamana. Kifungu hicho kinasema kuwa suala la kuuza mali ya dhamana kwa bei inayokubalika ni haki ambayo aliyeshindwa kulipa deni anamdai muuzaji/mnadishaji. Kwa hiyo wewe unayedaiwa unamdai huyo mnadishaji anayetaka kuuza nyumba yako haki ya kuuza hiyo nyumba katika bei inayokubalika ( reasonable price).
2. NYUMBA/KIWANJA KIUZWE BEI GANI KWA MUJIBU WA SHERIA ?
Sheria ya ardhi haikutaja moja kwa moja ni kiasi gani nyumba ya mtu au kiwanja kinatakiwa kuuzwa. Hii ni kutokana na utofauti wa thamani wa mali hizo na hivyo isingekuwa rahisi kusema kuwa bei ya mwisho ya nyumba au kiwanja ni kiasi fulani. Ili kuliweka sawa hili kifungu hichohicho cha 133( 2 ) kikasema kuwa nyumba/kiwanja cha mtu hakitakiwi kuuzwa 25% ya bei ya soko ya nyumba au kiwanja hicho kwa wakati huo au chini yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...