Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ameridhia pendekezo la wananchi wa jimbo lake kumuona Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kufuatia mapigano ya wakulima na wafugaji yaliyotokea wiki iliyopita ambapo watu watatu walipoteza maisha huku wengine wengi wakijeruhiwa baada ya wafugaji kulishia mifugo yao kenye Mazao ya wakulima katika mashamba yaliopo bonde la mgongola.

Kutokana na hali hiyo Mbunge kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama waliitisha mkutano wa hadhara kijiji cha Kugugu kuongea na wakulima wanaolima katika bonde la mgongola pamoja na mambo mengine wananchi walimuomba Mbunge wao kuundwe Kamati ya kumuona Waziri Mkuu kuhusiana na mipaka ya bonde la Mgongola ambalo limekuwa Mahakamani kwa zaidi ya miaka 15 na machafuko ya mara kwa mara yametokana na bonde hili kwa wafugaji wa kijiji cha Kambala kulishia mifugo yao kwenye Mazao ya wakulima na kupelekea uvunjifu wa Amani wa mara kwa mara.

Akiongea kwa niaba ya wananchi mkazi wa kigugu ndugu Salihina Mpenda alisema kuwa kesi ya bonde la mngongola umekuwa muda mrefu serikali haichukui hatua  watu wanaendelea kufa kila kukicha imefika wakati jitihada zako Mbunge ulizozifanya kuwaleta mawaziri 4, barua ulizomuandikia Waziri Mkuu na Waziri wa ardhi sisi wananchi tunakupongeza ila inapaswa tukuongezee nguvu tukamuone Waziri mkuu.

Akijibu hoja hiyo Mbunge na Naibu Waziri aliridhia ombi lao la kuundwa Kamati ya wakulima ya kumuona Waziri mkuu na akawataka wachague watu kumi na yeye kama Mbunge atagharamia gharama zote.

Aidha kwa upande mwingine Mkuu wa Wilaya hiyo,Festo Kiswaga amewahakishia hali ya usalama ndani ya bonde la Mgongola ni shwari wakulima waendelee na shughuli na Ulinzi wa Askari wa doria umeimarishwa.
Wananchi wa Jimbo la Mvomero wakimpongeza mbunge wao Amos Makalla kwa kukubali kufadhili Kamati ya kwenda kumuona Waziri Mkuu.
Wananchi Jimbo la Mvomero wakimpokea Mbunge wao, Amos Makalla aongee na wakulima bonde la Mgongolwa.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla akiongea na wananchi nje ya kituo cha polisi kuwa mahabusu wapo salama.
Mbunge wa mvomero akimpa pole na Fedha za matibabu mmoja wa wakulima aliyejeruhiwa kwa kuvunjwa Mkono.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2015

    kumwona waziri mkuu ya nini? wewe ni kiongozi wao kwanini usisikilize matatizo yao?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...