MAZISHI ya aliyekuwa msanii wa muziki wa asili Chigwele Che Mundugwao, 46, aliyefariki dunia jana asubuhi katika hospitali ya taifa Muhimbili, yanatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa  Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.

Rais
 wa Shirikisho la Muziki Tanzania Ado Novemba, alisema marehemu alifikwa na umauti huo baada ya kufikishwa hospitalini akitokea Keko gerezani ambako alikuwa mahabusi.
“Marehemu Che Mundugwao alikuwa akisumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu miezi miwili iliyopita, akiwa huko alipelekwa katika hospitali ya Amana na kugundulika na tatizo hilo. Mpaka sasa bado hatujafahamishwa chanzo cha kifo chake,” alisema Novemba.
Naye Makamu wa shirikisho hilo Samuel Mbwana alisema, “Che Mundugwao alilazwa katika hospitali ya Amana kwa kipindi cha miezi miwili kabla ya kurudishwa mahabusu na baadaye alipelekwa katika hospitali ya Muhimbili ambako alilazwa kwa muda kabla ya umauti kumfika leo saa moja asubuhi. Taarifa za mwisho za marehemu bado hatujazipata. Na ukizingatia alikuwa chini ya ulinzi hivyo bado hatujajua.”
Chigwele Che Mundugwao aliyekuwa ofisa Manunuzi  wa Idara ya Uhamiaji na wenzake watatu walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam mapema mwaka jana, wakikabiliwa na mashtaka manne likiwemo kosa la wizi wa  Pasipoti 26.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...