Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, Mhe. David Kafulila akihakikisha vitanda vilivyotolewa na mfuko wa jimbo lake katika kituo cha afya cha Nguruka, vinafungwa vyema.
Na Editha Karlo wa Globu ya jamii, Kigoma
Mfuko wa Mbunge wa Jimbo la Kigoma kusini, Mhe. David Kafulila umetoa magodoro 20 na vitanda 20 kwa kituo cha afya cha Nguruka ili kuboresha huduma ya afya kituoni hapo hasa kwa akina mama wajawazito.
Mganga Mkuu wa kituo cha afya Nguruka, Dk. Stanford Chamgeni alisema kuwa kituo hicho kilikuwa na jumla ya vitanda 25 na vingi vilikuwa ni vibovu,hivyo kupatikana kwa vitannda hivyo vipya vitapunguza tatizo la wagonjwa kulala 2 hadi 3 katika kitanda kimoja.
Dk. Chamgeni alisema kuwa kituo cha afya Nguruka pia kinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa wodi ikilinganishwa na wagonjwa wanaotibiwa kituoni hapo na kulazwa pia.
.jpg)
''Hapa sisi kwa mwezi tunaweza kutibu wagonjwa 200 wa ndani na wa nje sasa kutokana na upungufu wa wodi inatulazimu wagonjwa wanaolazwa wengine kulala kitanda kimoja wawili hadi watatu ambayo kiafya si hali nzuri''alisema Dk. Chamgeni
Alisema hali mbaya zaidi ipo katika wodi ya akina mama ina vitanda saba tu hivyo inawalazimu kuwalaza wagonjwa wote wanawake mchannganyiko yaani waliojifungua,wanaosubiri kujifungua na wenye matatizo ya uzazi.
Naye Mbunge wa jimbo hilo Mhe David Kafulila alisema kuwa atashirikiana na uongozi wa kituo hicho ili kuhakikisha changamoto zote zilizopo kituoni hapo zinapata ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kuiomba serekali kituo hivho kipate hadhi ya Wilaya.
''Kwaweli wagonjwa ni wengi ambao wanazidi uwezo wa kituo,kazi kubwa ninayo ifanya ni kuisukuma serekali ili ikipandishe hadhi kituo hiki na kuwa kituo cha Wilaya ili huduma nyingi za afya ziwekupatikana''alisema Kafulila
Pamoja na msaada huu mkakati wa kupanua hospitali hii hunatakiwa uwepo kwa sababu ya idadi kubwa ya wagonjwa.
ReplyDeleteTunamshukuru Mungu janga la Ebola linapungua Afrika yale waliyopitia wenzetu Afrika magharibi yatufundishe Kuimarisha huduma katika vituo vya afya, zahanati na hospitali zetu.