Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla Aprili 3,2015 alichangiwa fedha kiasi cha sh 2,319,500 na wananchi wa kijiji cha Manyinga na vijiji vya jirani kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania Ubunge mara muda utakapofika.
Tukio la kuchangiwa fedha za kuchukulia fomu lilichagizwa na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Stephen Kebwe aliyefanya ziara ya kukagua hospitali teule ya Bwagala na kisha kuongea na wananchi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara.
Alipopanda jukwaani, Dk. Stephen Kebwe alisema "nionavyo mnafuraha sana na mnampenda sana Mbunge wenu", wananchi wakamjibu kwa sauti Makalla ni jembeee.
Kusikia hivyo, Dk. Kebwe akawatania kama kweli mnampenda Amos Makalla basi onyesheni kwa kumchangia ili achukue fomu, hapo ndipo umati ulipolipuka na kuanza kuwasilisha michango.
Akiwashukuru wananchi hao, Mbunge wa Mvomero alisema amepokea msaada huo kwa heshima kubwa na kwa maana kubwa ikiwepo imani kubwa waliyoonyesha wananchi hao kwake.
Amewaahaidi kugombea tena Ubunge na zaidi amewaomba ushirikiano na amewahakikishia utumishi uliotukuka.
Aidha katika tukio lingine amewakabidhi Wawakuda Saccos ya Kijiji cha Dakawa msaada wa computer na printer yenye thamani ya sh 2,000,000 .
Akishukuru Mwenyekiti wa Wawakuda Saccos, ndg. Mohamed Mkupete alimshukuru sana mbunge kwa msaada wa computer ambayo walimuomba wiki moja iliyopita na leo ametembelea"mheshimiwa Makalla wewe ni mtu makini na huna longolongo ndani ya wiki moja umetekeleza tunakushukuru sana".
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Stephen Kebwe akiwa na Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla wakiongozana wakati wakiwa kwenye ziara ya kutembelea hospitali teule ya Bwagala, Turiani Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Stephen Kebwe akiwa na Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla wakiwajualia hali wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Stephen Kebwe akipokea mchango wa wananchi wa Jimbo la Mvomero waliomchangia Mbunge wao wa Mvomero, Amos Makalla ili achukua fomu za kuwania Ubunge wa Jimbo hilo wakati utakapofikia.
Kwa nini wamchangie?
ReplyDelete