![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Kagera wa sasa Mheshimiwa John V.K. Mongella ukimuaga aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Kagera wa 20 Kanali Mstaafu Fabian Inyasi Massawe kwa jina maarufu Mulokozi. |
Viongozi hao (Wakuu wa Mkoa) waliowahi kuuongoza mkoa wa Kagera kwa
nyakati tofauti waliweza kuisogeza Kagera kutoka katika hali
fulani na kupiga hatua kimaendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchumi,
elimu, siasa, utamaduni, miundombinu, na
nyanja mbalimbali za ustawi wa jamii.
Mkoa wa Kagera chini ya uongozi
wa Mkuu wa Mkoa wa sasa Mheshimiwa John V.K. Mongella ulimuaga aliyekuwa Mkuu
wa Mkoa Kagera wa 20 na aliuongoza
mkoa kwa miaka mitatu akiteuliwa
kutoka katikanafasi ya Ukuu wa Wilaya ya Karagwe naye ni Kanali Mstaafu Fabian Inyasi Massawe kwa jina maarufu Mulokozi.
Kama walivyokuwa watangulizi wake
Mhe. Kanali Mstaafu Massawe alifanya mengi katika mkoa wa Kagera na kuweka
rekodi ya mambo mengi aliyoyafanya yakiongozwa na kaulimbiu yake ya “Amani
na Maendeleo” kubakia katika kumbukumbu za mkoa wa Kagera na
wananchi wake kwa ujumla.
Kupata historia ya Kanali Mstaafu Fabian Inyasi Massawe BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...