Aprili Mosi kila mwaka huwa ni siku ya kupanda miti kitaifa na mwaka huu 2015 mkoa wa Kagera ulipewa heshima ya kuadhimisha siku hiyo ambapo iliadhimishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi na kushirikisha wadau mbalimbali pamoja na wananchi wanaojihusisha na kupanda miti na kutunza misitu.

Maadhimisho hayo yaliyoongozwa na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Celestine Gesimba kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo maadhimisho hayo yalianzia katika Kijiji cha Bugolola eneo la Omukajunguti kwa kupanda miti 2100 kwa kushirikisha washiriki wote na wananchi wa kijiji hicho.

Kauli mbiu ya siku hiyo ilikuwa ni “Misitu ni Mali Panda Miti.” Katika Hotuba yake Naibu Katibu Mkuu Bw. Gesimba alisema wizara yake siyo kwamba inahamasisha wananchi kupanda miti ili kulinda mazingira tu bali wananchi wapande miti ili kunufaika nayo kwani ni mali inayoingiza kipato kikubwa kwa mwananchi mmoja mmoja.

Bw. Gesimba alisema wananchi wanatakiwa kupanda miti kwa wingi kwani miti isipopandwa itasababisha maafa makubwa hapo mbeleni kama inavyoanza kuonekana kwa sasa mfano, ukosefu wa mvua au mvua kutonyesha kwa wakati, joto jingi, kuyeyuka kwa theruji mlima Kilimanjaro.
Bw. Gesimba alimalizia hotuba yake kwa kusema kuwa kutotunza misitu kumesababisha baadhi ya sehemu kuwa jangwa au kusababisha ugonjwa wa malaria mfano Lushoto mkoani Tanga ambako hakukuwa na ugojwa huo miaka ya 1970 na 1990. Aidha alitahadhalisha misitu kutoweka kabisa kwani   kila baada ya dakika sita (6) nusu kiolmeta ya misitu hutoweka duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hili eneo linahitaji miti pandeni miti asilia na ya muda mfupi kuzuia hali ya jangwa na kupata bidhaa za misitu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...