Jumuia ya watanzania Wasabato walioko Marekani (Tanzania Adventists
in the United States), kwa kifupi TAUS, itakuwa na mkutano mkubwa wa
kiroho (TAUS Retreat 2015) unaoanza leo Washington DC. Viongozi wa TAUS
wanawakaribisha watu wote wajumuike pamoja nao katika kumsifu na
kumshukuru Mungu muumbaji wetu.
TAREHE ZA MKUTANO: April 16 (saa 11 jioni), mpaka April 19 (saa 5 asubuhi)
MAHALI- Burnt Mills SDA Church; 10915 Lockwood Drive, Silver Spring MD 20901
MGENI RASMI: Mchungaji Wilbert Nfubhusa toka Kigoma, Tanzania.
MOTO: Kufanana na Yesu
Mbali
na neno la Mungu, mafundisho ya ndoa, malezi bora ya watoto, kutafuta
wachumba na mengineyo yatatolewa. Pia kutakuwa na kwaya na vikundi
kadhaa vya uimbaji. Vyakula na vinywaji baridi vitatolewa kwa wote.
Karibuni sana, na Mungu awabariki
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...