Shirika
la fedha la kimataifa (IMF) hujishughulisha na kutoa ushauri wa kisera kwa nchi
wanachama na kutoa mikopo na misaada ya kifedha. Waziri wa Fedha Mhe. Saada
Mkuya Salum aliyaeleza hayo mjini hapa.
Akishiriki kikao cha kundi la Africa(African Group one Constituency). Kundi hili hukutana kila kunapokuwa na mikutano ya Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia kwa lengo la kuwezesha nchi za Afrika kuwa na sauti moja na kujua hatua ambazo Nchi za Afrika zimefikia kuhusiana na Taasisi zake za kifedha.
Mhe.
Mkuya alichangia mada mbalimbali zilizohusu kundi hilo akilenga zaidi maendeleo
na muelekeo mzuri wa mafanikio ya kifedha katika nchi ya Tanzania.
Waziri wa Fedha wa Tanzania Mhe. Saada Salum Mkuya ni
Gavana katika mkutano huu akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ambaye ni Gavana
msaidizi kwa upande wa Benki ya Dunia (WB), aidha Gavana wa Benki kuu
Prof. Benno Ndulu ni Gavana msaidizi kwa upande wa Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF).
Katika Mkutano huu
Magavana hawa ndio wenye maamuzi ya juu na nguvu kubwa ya kuweza kuyashawishi
mashirika ya kifedha kuhusu nini kifanyike. Mkutano huu uliofanyika
leo, umeangalia uhalisia na vigezo vinavyotolewa na Shirika la Fedha la kimataifa
katika kuimarisha taasisi za kifedha katika nchi wanachama Afrika.
Katika
mkutano huu, mambo muhimu yaliyojadiliwani pamoja na maendeleo katika kundi
hilo na mabadiliko ya maboresho katika Benki ya Dunia. Wakijadiliana katika
mkutano huo wajumbe hao wameshauri Shirika la fedha la kimataifa pamoja na
taratibu zake, liangalie namna ya kulegeza masharti ya mikopo ili nchi
wanachama ziweze kufanya mabadiliko ya kifedha kwa urahisi.
Mikutano
hiyo bado inaendelea hapa mjini Washington DC. na nchi wanachama wanaendelea
kufika kwa wingi.
Ujumbe kutoka Tanzania ukifuatilia kwa karibu mkutano huu. (African Group one Constituency
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akishiriki katika mkutano huu wa kundi la Afrika. (African Group one Constituency)
Ujumbe kutoka Tanzania ukifuatilia kwa karibu mkutano huu. (African Group one Constituency)
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...