Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick, ameitaka  Bohari ya Dawa MSD kuendeleza kasi ya huduma zake za kupambana na ugonjwa wa malaria kwakuwa ni  moja ya taasisi  zilizo mstari wa mbele kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa huo.
Akizungumza jana katika banda la MSD ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Malaria duniani Sadick alisema MSD imekuwa ikifanya jitihada kuhakikisha ugonjwa wa malaria unakoma na vifo vitokanavyo na ugonjwa huo vinapungua.
Alisema jitihada hizo za MSD zimechangia matokeo ya kupungua takwimu za vifo vya mama na mtoto mchanga chini ya miaka mitano vitokanavyo na ugonjwa wa malaria hivyo jitihada zaidi zinahitajika kuhakikisha malengo ya millennia ya kupunguza vifo hivyo yanafikiwa.
Alisema kutokana na MSD kuhakikisha dawa za malaria zinapatikana katika kila kituo cha afya, Zahanati na Hospitali ni wajibu wa wananchi kuhakikisha wanafanya  matumizi sahihi ya dawa hizo ili kutibu ugonjwa huo.
“MSD inasaidia serikali kufikia lengo la kupunguza ugonjwa wa malaria tumeelezwa jinsi gani MSD inahakikisha dawa za malaria hazikosekani katika vituo vya kutolea huduma lakini pia imepanua  wigo kwa kutoa elimu kwa vitendo jinsi ya kupambana na ugonjwa huo kwa  kuhakikisha kinga dhidi ya malaria   inaanzia kwa wafanyakazi wake na wanapewa vyandarua vyenye dawa wao na familia zao,”alisema
Sadick aliwataka wananchi kuacha kutumia dawa hizo katika matumizi yasiyo sahihi ikiwemo dozi moja ya dawa kutumiwa na watu zaidi ya mmoja kwakuwa kufanya hivyo kunasababisha matibabu ya wagonjwa wa malaria kutokukamilika na kusababisha vifo.
Alisema pia kumekuwepo na matumizi yasiyo sahihi  katika vyandarua vya msaada ambapo utumika kwa ajili ya kufugia Kuku au kuvulia Samaki hivyo mapambano dhidi ya ugonjwa huo kutokufanikiwa.
“ Jitihada hizi za MSD na wafadhili mbalimbali katika kuweka  nguvu ya  kupambana na Malaria ni wajibu wa  jamii kuziunga mkono kwakuwa matumizi ya misaada hiyo ikiwemo Vyandarua ikitumiwa  kwa malengo yaliyokusudiwa  kutaongeza uzalishaji wa uchumi katika nchi kutokana na kuimarika kwa afya ya wananchi wake,”alisema.
Katika maadhimisho hayo Mkuu Mkoa huyo alizindua mpango wa ugawaji wa Vyandarua milioni 24 kwa nchi mzima ikiwa ni jitihada za Serikali na wadau mbalimbali kupambana na ugonjwa wa Malaria.
 Ofisa wa Kitengo cha Udhibiti Ubora wa MSD, Richard Makalla (kulia), akimuelekeza jambo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki alipotembelea banda la MSD katika maadhimisho hayo. Kushoto ni Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam wa MSD, Florida Sianga na ofisa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa.
 Muenekano wa banda la MSD katika maadhimisho hayo.
 Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam wa MSD, Florida Sianga (kushoto), akimuelekeza jambo kijana aliyetembelea banda la MSD katika maadhimisho hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...