Katika kuadhimisha sikukuu ya Pasaka kwa furaha,wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake wataweza kupata burudani za aina mbalimbali katika tamasha kubwa la Pasaka litakalofanyika katika ufukwe wa maraha wa Coco beach chini ya maandalizi ya Vodacom Tanzania.
Akiongea juu ya tamasha hili kubwa ambalo hivi sasa limeanza kuwa gumzo ya jiji,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu alisema mipango yote kuhusiana na tamasha hilo imekamilika kinachongojewa ni kuwasha moto wa burudani kwa wateja wa Vodacom na wananchi wote kwa ujumla.
“Kama ilivyo kawaida yetu ya kuwapatia huduma bora wateja wetu sambamba na kuwaburudisha zamu hii tumewaandalia tamasha hili ili waweze kuburudika katika kuadhimisha sikukuu ya Pasaka ambapo pia watapata fursa ya kukutana na wasanii mbalimbali wawapendao na kuwa karibu nao ukiwa ni mwendelezo wa promosheni ya Vodacom ya kuleta burudani kwa wateja inayojulikana kama Ishi Kistaa”.Alisema.
Nkurlu alisema kuwa tamasha hilo litakalofanyika siku ya Jumapili ya Pasaka litaanza asubuhi saa tano kwa burudani mbalimbali za muziki na michezo kwa ajili ya watoto ambapo baadaye jioni wasanii mbalimbali wa bongofleva na aina nyingine ya muziki watapanda jukwaani kutoa burudani kwa washabiki watakaohudhuria kwenye tamasha hilo.
Alisema wako wasanii wengi wamejipanga kutoa kuburudisha wapenzi wa muziki baadhi yao wakiwa ni Shilole na Bob Junior na wengineo. “Wateja na mashabiki watapata fursa ya kuonana na mastaa ambao wanawapenda pia tunawakumbusha wachukie nafasi ya kushiriki katika promoshe ya Ishi kistaa kwa kutuma neno STAR kwenda 15670”.
Alimalizia kwa kusema kuwa hali ya amani na usalama inatarajiwa kutawala kwenye tamasha hili kwa kuwa kuna ulinzi wa kutosha kuhakikisha wananchi wanapata burudani murua kwa utulivu wakiwa na familia zao na aliahidi kuwa wateja wa Vodacom na wananchi wengine wanaokaa mbali na Dar es Salaam wakae mkao wa kula kwa kuwa mikakati inaandaliwa kupeleka burudani za aina hii katika sehemu mbalimbali nchini kwenye sikukuu mbalimbali zijazo katika siku za usoni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...