NA MWANDISHI WETU,
MEYA wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda amekabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali vyenya thamani ya shilingi milioni 2.5 kwa vikundi vitatu vya kulea watoto yatima, Dar es Salaam jana kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Pasaka.

Akikabidhi msaada huo Meya Yusuph Mwenda aliwataka watanzania kuwa na moyo wa kusaidia watoto hao hususan katika msimu wa Sikukuu ikiwa ni njia mojawapo ya kuwafariji watoto hao.

“Hakuna anayependa kuona watoto hawa wanaongezeka mitaani, Na Serikali inafanya juhudi kubwa kuondoa tatizo la watoto hawa hasa wanaotelekezwa mitaani lakini peke yake haiwezi, ni lazima wananchi muunge mkono juhudi hizo.” Alisema Mwenda.

Alisema kuwa badala ya watu kusherehekea Sikukuu majumbani mwao ni vema wakajumuika na watoto hao ili kuwafanya nao wajisikie wapo na wazazi wao. 

Msaada aliotoa Meya huyo ni pamoja na Mchele, Sukari, Mafuta, Unga wa Ngano, Unga wa Sembe, Sabuni za miche na unga, Mbuzi na vitu vingine.
Meya Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akikabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa watoto wa kituo cha kulea watoto yatima cha Kiwohede- Bunju kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, kwenye hafla iliofanyika Manispaa hiyo, Dar es Salaam jana.
Meya Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akikabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa watoto wa kituo cha kule watoto yatima cha Malaika kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, Dar es Salaam jana.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa vikundi hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...