Waandishi
wa habari hapa Nchini wametakiwa kuwaelimisha jamii juu ya umuhimu wa
amani katika nchi ya Tanzania tunapoelekea uchaguzi mkuu kwa kuandika na
kutangaza amani hali itakayosaidia uchaguzi kufanyika kwa amani
Akizungumza
katika mkutano wa siku mbili wa kujadili masuala ya ulinzi na usalama
kuelekea uchaguzi mkuu,uliofanyika jijini Arusha mwisho mwa wiki,
ulioandaliwa na mtandao wa utetezi wa haki za binadamu. Mkuu wa Wilaya
ya Arumeru mkoa Arusha Husna Mwilima alisema kuwa uvunjifu wa amani una
madhara makubwa sana katika nchi
Alisema
kuwa vyombo vya habari vinajukumu kubwa la kuelimisha umma madhara ya
vita hasa tunapoelekea uchanguzi mkuuu wa Rais,wabunge na madiwani,huku
akitaka Tanzania kuiga mfano wa Kenya ambapo vyombo vya habari vya nchi
hiyo vilikuwa vikitangaza na kuandika amani kipindi cha uchaguzi
Mwilima
amewaomba viongozi wa vyama vya siasa, dini na taasisi zisizo za
kiserikali kushirikiana kueleza wafuasi wao juu ya umuhimu wa kutunza
amani wakati wa uchaguzi mkuu.
Kwa
upande wake Mratibu wa Mtandao wa Kutetea Haki za binadamu Onesmo Ole
Ngulumwa alisema kuwa marekebisho ya baadhi ya mambo kabla ya uchaguzi
mkuu ni muhimu ili kufanyika uchaguzi salama na yenye kujali demokrasia
Pia aliongeza kuwa kwa kuwepo kwa amani itasaidia sana wananchi kupiga
kura katika hali ya kiusalama zaidi.
Mkuu
wa Wilaya ya Arumeru Husna Mwilima aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Arusha,
Daudi Ntibenda,akifungua mkutano wa kujadili masuala ya ulinzi na
usalama kuelekea uchaguzi mkuu, ulioandaliwa na mtandao wa utetezi wa
haki za binadamu uliofanyika jijini Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel
wa jamiiblog)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...