Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahmani Kaniki akisalimiana na baadhi ya
Wakufunzi wa chuo cha Polisi Moshi (CCP) wakati alipokuwa katika ziara ya
kikazi kukagua mafunzo yanayoendelea chuoni hapo.Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho,
Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Matanga Mbushi.
Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahmani Kaniki (kushoto) akiwasili katika chuo
cha Polisi Moshi (CCP) wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua mafunzo
yanayoendelea chuoni hapo.Katikati ni Mkuu wa Chuo hicho, Kamishna msaidizi
mwandamizi wa Polisi (SACP) Matanga Mbushi na Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la
Polisi, Naibu Kamishna Omar Rashid (Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi)
Na Frank Geofray-Jeshi la
Polisi, Moshi.
Wakufunzi
wa Chuo cha Polisi Moshi (CCP) wametakiwa kuendelea kutoa mafunzo kwa weledi
ili kuweza kupata askari bora ambao watashirikiana na jamii katika kupambana na
uhalifu hasa katika kipindi hiki ambapo kumeibuka uhalifu mpya kwa njia ya mitandao
na unaovuka mipaka.
Wito
huo umetolewa jana mjini moshi na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki wakati alipokuwa
katika ziara ya kikazi chuoni hapo ambapo alizungumza na wakufunzi hao na
kuweka mikakati mbalilmbali ya kuboresha mafunzo katika chuo hicho.
Naibu
IGP Kaniki alisema, askari wakipata mafunzo bora wataongeza mbinu
zitakazowezesha kukabiliana na uhalifu
huo na hivyo kuendelea kuimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kushirikiana
na jamii ambayo imekuwa msaada mkubwa wa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.
“Ili
kuhakikisha kwamba raia wa Tanzania na mali zao wanalindwa ipasavyo, Jeshi la
Polisi hatuna budi kuendelea kubuni mbinu mpya za kukabiliana na uhalifu wa
kila aina unaobadilika mara kwa mara na hilo linawezekana kwa kuendelea
kuwapatia askari wetu mafunzo yenye viwango vya kupambana na uhalifu unaokua
kwa kasi”alisema Kaniki.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo cha Polisi moshi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) Matanga Mbushi alisema wanaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa
mafunzo wanayotoa yanalenga katika mitaala ambayo wamekuwa wakiiboresha mara
kwa mara ili kuendana na wakati kulingana na mazingira ya uhalifu unaotokea
katika jamii.
Alisema,
mbinu za uhalifu zimekuwa zikibadilika kila siku hivyo, na wao kama chuo wamejikita kuhakikisha kuwa askari wanaopita
katika chuo hicho wanazipata mbinu mpya na hivyo kuwa zaidi ya wahalifu ili
waweze kupambana nao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...