Wakati Mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la kifedha la kimataifa ikiendelea hapa Mjini
Washington Dc. Mawaziri wa fedha wameweka misimamo yao juu ya sera ambazo zinawekwa
na Benki ya Dunia.
Akizungumza na vyombo vya habari,waziri wa fedha wa Tanzania Mhe. Saada Salum Mkuya
alisema” Sisi kama nchi tuliwasilisha nini tunaona katika utekelezaji wa mipango ya Benki.
Tumeshukuru sana Benki ya Dunia kwa kuendeleza mipango ya kuweza kusaidia nchi za
kiafrika ,hususan kwenye mipango ya kujenga miundo mbinu ya kiuchumi kama vile barabara,
kilimo pamoja na miundo mbinu ya maji na umeme”.
“Lakini vilevile tumeonyesha wasiwasi wetu kutokana na sera ambazo Benki ya Dunia
imeziweka, kama vile kuangalia sera zile za watu wa kiasili ya kiafrika, sisi tumehisi mbali ya nia
nzuri na njema ya Benki hii ya Dunia, lakini inaweza kuwa ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo
ya nchi zetu kwa sababu sera hiyo inaweza kutumika kuigawa nchi ambayo misingi yake
imekuwa ikijengwa kwa umoja kutoka uhuru”.Alisistiza Mkuya.
Hakuishia hapo aliendelea kutoa mfano kuwa “sisi watanzania tumekuwa wamoja ingawa tuna
lugha mbalimbali kutokana na makabila tofauti. Lakini tumekuwa pamoja kwa kipindi cha miaka
50.Kwa hiyo tumeona sera hiyo isije ikatumika kwa ajili ya kuwa kigezo cha utekelezaji wa
miradi ya maendeleo nchini . Sisi kama wa Afrika na viongozi wa Afrika tunashirikiana kuona
kuwa sera zinazowekwa hazitukwamishi”.
Hali hii ya kudai uasilia (indigenous) imeibuka zaidi katika miongo hii miwili, wakati kukiwa
kumejitokeza watu wanaodai kuwa wao hawatambuliki na hoja hii inaihusu hasa nchi ya
Tanzania.
Mawaziri wa Fedha kutoka Afrika wamejadili mambo mbali mbali ambapo ni pamoja na masuala
ya maendeleo na mahusiano yao na Benki ya Dunia.
Katika Mkutano huo wa kisheria Mkurugenzi Mtendaji ndiye ambaye amewasilisha maazimio
ya Benki katika kipindi cha miezi sita.Aliongeza Mkuya.
Aidha katika mkutano huo pia walizungimzia suala la Ebola. “Kwa kweli wamekubali kusaidia
nchi zile ambazo zimekumbwa na gonjwa hili lakini wamezitaka nchi za afrika na zenyewe
kushirikiana katika kupambana na gonjwa hili”.Alimalizia Mkuya.
Mikutano hiyo bado inaendelea hapa mjini Washington DC. Hali ya hewa ni baridi kiasi.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile kushoto kwake kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa kisheria wa kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa kisheria kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile kushoto kwake kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa kisheria wa kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile kushoto wakifuatilia semina iliyokuwa ikitolewa kuhusu uimarishaji wa makazi mijini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...