Waziri wa Mambo ya Nje wa Zamani wa Marekani Mama Hillary Clinton akiwa na wenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa Ikulu Dar es salam wakati alipotembelea Tanzania June 13, 2011.
Imetangazwa leo kuwa Mama Clintoameamua kujitosa katika kuwania nafasi ya Urais wa nchi hiyo mwakani. John Podesta, Meneja wa kampeni wa Clinton leo katuma email kwa wanaomuunga mkono, kwamba Clinton yumo katika mbio hizo,
Podesta amesema Clinton anaelekea Iowa kukutana na wapiga kura na kwamba sherehe rasmi ya kutoa tamko itafanyika mwezi ujao.
Akiongea kwenye video fupi iliyo kwenye tovuti yake rasmi ya kampeni, amesema" Mimi natagombea urais, Wamarekani wamepigana na kigingi cha hali ngumu ya uchumi lakini karata bado iko mikononi mwa walio juu. Kila siku Wamarekani wanahitaji bingwa, nami nataka kuwa huyo bingwa ili tuweze kufanya zaidi ya kupita tu. Inawezekana kuwa mbele na kubakia mbele, Sababu pale familia zinapokuwa na nguvu, Marekani ina nguvu.
"Hivyo naingia barabarani kupata kura zenu, Sababu huu ni muda wenu na namini mtaungana nami katika safari hii" amesema kwenye video hiyo ambayo ukitaka kuiona kwenye tovuti yake....
Hata wakina mama nao wanaweza mwache apambane, ana ujuzi na uzoefu wa kutosha akipata anaweza kuwa kiongozi mzuri tu wa nchi kubwa.
ReplyDelete