Ikiwa moja kati ya huduma zake za ‘Corporate Social Responsibility’ kwa jamii zitolewazo na NexLaw Advocates tarehe 4 April 2015 NexLaw Advocates ilitembelea vituo viwili vya watoto jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka. 
Vituo vilivyotembelewa na kampuni ya NexLaw Advocates ni House of Blue Hope ya Mabibo ambacho ni kituo cha kulelea watoto yatima na wasiojiweza na kituo cha watoto cha Msimbazi Children’s Home Centre cha Msimbazi jijini Dar es Salaam Home Centre. 
 NexLaw Advocates ilitoa mchango wa vifaa vya shule, vyakula pamoja na vifaa vingine vya usafi kwa kituo cha watoto cha House of Blue kilichopo Mabibo, Dar es Salaam. Na katika kituo cha watoto cha Msimbazi Children Home Centre wafanyakazi wa NexLAw Advocates walipata chakula cha mchanapamoja na wafanyakazi wa kituo hicho pamoja na kutoa Zawadi mbalimbali zikiwemo matunda, vyakula na Zawadi zingine ndogondogo. 
 Shughuli hizi mbili zilichochewa na dhima ya NexLaw Advocates kitengo cha ‘Corporate Social Responsibility’ kuhakikisha kuwa inatambua mchango na kuunga mkono shughuli zinazofanywa na taasisi, vikundi na watu binafsi katika kuwasaidia na kuwalea watoto na vijana wasiojiweza na walio kwenye mazingira magumu. 
 Katika vituo hivyo vitu mbalimbali vilitolewa ambapo katika kituo cha Msimbazi Children’s Home Centre kulikuwa na chakula cha mchana pamoja na wafanyakazi wote. Ikiwa ni moja ya sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii , kukumbuka na kuthamini mchango wa wafanyakazi wanaowalea na kuwaangalia watoto katika vituo vyote. 
Pia kama mchango kidogo ofisi ilinunua zawadi mbalimbali kwa ajili ya watoto na wahudumu katika vituo vyote viwili.
 Baadhi ya wafanyakazi wa NexLaw Advocates chini ya jengo  la PPF TOWER (Zilipo ofisi za kampuni hiyo) wakipakia vitu kwenye gari kabla ya kuanza safari kuelekea Vituo viwili vya kulelea watoto ambavyo ni House of Blue Hope kilichopo Mabibo na Msimbazi Children’s Home vilivyopo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa NexLaw Advocates wakielekea kukabidhi bidhaa zilizopelekwa Msimbazi Children’s Home  Centre cha Msimbazi jijini Dar es salaam
 Baadhi ya wafanyakazi wa NexLaw Advocates wakielekea kukabidhi bidhaa zilizopelekwa Msimbazi Children’s Home  Centre cha Msimbazi jijini Dar es salaam
 Sister Anna Francis mlezi wa kituo cha watoto cha Msimbazi Children’s Home wakijadili jambo na wafanyakazi wa NexLaw Advocates.
 Wafanyakazi wa NexLaw Advocates wakipata chakula cha mchana pamoja na wafanyakazi wa Msimbazi Children’s Home Centre. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...