Shirika la Bima la taifa leo limetoa msaada wa vifaa 34 vya kujifunzia darasani kwa watoto wenye uoni hafifu katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi(Albino),wasioona na wasiosikia cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga. Vifaa vilivyotolewa ni darubini kiona mbali(Telescope Monocular),Kikuza Maandishi cha Kusimamisha(Stand Magnifier) na Kikuza Maandishi cha Kuweka juu ya Maandishi( Dome Magnifier)-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Ndani ya ofisi ya mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Bungaja ambaye ndiye msimamizi mkuu wa kituo cha walemavu wa ngozi,wasioona na wasiosikia cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga,Mwalimu Peter Ajali (katikati),wa kwanza kushoto ni Meneja wa Shirika la Bima la taifa tawi la Shinyanga Halima Makange ,kulia ni Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez wakijadili jambo kabla ya kukabidhiana vifaa 34 vilivyotolewa na Shirika la Bima la taifa ikiwemo Darubini kiona mbali(Telescope Monocular),kikuza maandishi cha Kusimamisha(Stand Magnifier) na Kikuza Maandishi cha Kuweka juu ya Maandishi( Dome Magnifier).
Meneja wa Shirika la Bima la taifa tawi la Shinyanga Halima  Makange akimkabidhi  vifaa hivyo na kushikana mkono na msimamizi mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...