Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (katikati),akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa kutangaza ushirikiano wa kimkakati na Benki Tarajiwa ya Walimu (Mwalimu Commercial Bank in-formation) kurahisisha ununuaji hisa kupitia huduma ya M-Pesa pamoja na kampuni ya Maxcom Africa kupitia huduma yake ya Maxmalipo, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ronald Manongi na kulia ni Ofisa Mkuu wa Maswala ya Biashara wa Max Malipo Ahmed Lussasi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mwalimu Commercial Bank (in-formation), Ronald Manongi na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kushoto) wakipeana mikono ikiwa ishara ya uzinduzi wa ushirikiano wa kimkakati na Benki hiyo kurahisisha ununuaji hisa kupitia huduma ya M-Pesa pamoja na kampuni ya Maxcom Africa kupitia huduma yake ya Max Malipo. Wengine katika picha wapili kushoto ni Ofisa Mkuu wa Maswala ya Biashara wa Max Malipo Ahmed Lussasi na Mwekahazina Mkuu wa Benki hiyo Nunu Saghaf.
Dar es Salaam, 22 Aprili, 2015 – Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ambao ni waanzilishi wa Benki Tarajiwa ya Walimu (Mwalimu Commercial Bank in-formation), kinawatangazia Walimu na Watanzania wote kwa ujumla juu ya uuzwaji wa Hisa za Benki tarajiwa ya Walimu, kwa lengo la kupanua wigo wa wanahisa na kuongeza mtaji ulianza tarehe 23 Machi 2015 na unategemea kumalizika tarehe 4 Mei 2015.
Ili kufikia azma hii, pamoja na njia nyingine za uuzaji wa Hisa zake, Benki Tarajiwa ya Walimu inatangaza ushirikiano wa kimkakati na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kupitia huduma yake ya M-Pesa pamoja na kampuni ya Maxcom Africa kupitia huduma yake ya Maxmalipo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...