Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo ya 55 ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo iliyofanyika leo,ambapo Habibu Saidi(19)ambaye ni mkazi wa Kabale Bukoba vijijini anayesubiria kuanza kidato cha tano hivi karibuni kwa kujishindia kitita cha shilingi milioni 10.Kutoka kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544 au AUTO kwenda namba hiyo iwapo simu haina fedha ambapo  mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-tu.

Zaidi ya milioni 300/-zimesha nyakuliwa na wateja walioshinda
Watanzania wapatao 44  maisha yao yameweza kubadilika kutoka hali ya kawaida na kuwa mamilionea kutokana na kujishindia fedha taslimu kupitia promosheni ya siku 100 ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania ambayo ilianza katikati ya mwezi Februari na inatarajia kufikia ukingoni mapema mwezi ujao.
Hadi kufikia sasa wateja wa Vodacom walioshinda wamejinyakulia shilingi milioni 278 huku mamilioni mengine ya fedha yakisubiri kunyakuliwa na washindi watakaobahatika katika siku chache zilizobaki kabla ya promosheni kufikia tamati.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema promosheni bado inaendelea na kuwataka watanzania waendelee kuangalia  namba zao kama zimeshinda kwa kutuma neno JAY kwenda namba 15544. Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo  mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-

“Promosheni ya Jaymillions inaendelea hivyo tunawakumbusha wateja wetu kuwa bado kuna mamilioni ya kujishindia hivyo wachangamkie kwa kujaribu bahati zao katika siku hizi ambazo promosheni inaelekea ukingoni.Tunajivunia kwa kufanikiwa kubadilisha maisha ya baadhi ya wateja wetu walioshinda wengi wakiwa ni wateja wenye maisha ya kawaida na hii ndio dhamira yetu kubwa inayoendana na kauli mbiu yetu ya “ukiwa na Vodacom maisha ni murua”. Nkurlu alisema hayo wakati wa kuchezesha droo ya 55 iliyomwibua Habibu Saidi(19)ambaye ni mkazi wa Kabale Bukoba vijijini anayesubiria kuanza kidato cha tano hivi karibuni kwa kujishindia kitita cha shilingi milioni 10.
Baadhi ya wateja waliobahatika kushinda wanasema kuwa promosheni hii imewafanya kutimiza ndoto zao zilizoshindwa kutimia kwa muda mrefu kwa kuwa maisha yao yamebadilika kutoka hali duni kuwa bora zaidi.
Upendo Madengenya kutoka wilayani Kilolo ambaye alikuwa mhudumu katika nyumba ya kulala wageni wilayani humo ambaye alijishindia milioni 100 anasema“Jaymillions naifananisha na methali ya Kiswahili ya kulala maskini ukaamka tajiri kwa kuwa nilikuwa nakabiliwa na changamoto nyingi za maisha pamoja na familia yangu ,Mungu kaniona nikafanikiwa kushinda hivi sasa maisha yangu yamebadilikakutoka hali duni kuwa bora na bado safari ya kuelekea kwenye maisha bora zaidi inaendelea.
James Mangu kutoka Mwanza ambaye alijishindia milioni 10 anasema kuwa kwa muda mrefu alikuwa anawaza kupata mtaji wa kuendeleza biashara zake ndogo ndogo na kwa bahati nzuri ameweza kuibuka na ushindi na kupata mtaji ambao anakiri kuwa utabadilisha maisha yake na familia yake kwa  ujumla kutoka maisha duni kuwa bora.
Hynes Petro Kanumba mkazi wa Rukwa anasema:”Katika maisha yangu sitaisahau Vodacom Kwa kuwa kupitia promosheni yake ya Jaymillions imeniwezesha kunitoa katika hali duni na kuwa na maisha bora pamoja na familia yangu na natoa wito kwa watanzania kutozipuuza promosheni hizi kwa kuwa ni za kweli na zinalenga kutukomboa sisi wanyonge”
Kwa upande wake Deborah Stanley mshindi wa milioni 10 anasema: “Nimefuatilia Promosheni ya Jaymillions naona inalenga kuwakomboa kimaisha watanzania hususani wenye kipato cha chini hasa  wajasiriamali wadogo wadogo kama vile; wamachinga, mama ntilie, wanafunzi na wazee wastaafu ambapo kwa kiasi kikubwa tunajua watu wa aina hii wanahitaji msaada ili kujiendeleza kiuchumi. Kwa fedha ambazo baadhi ya washindi tayari wamezipata wengi zimewasaidia kujikwamua na kujiendeleza kimaisha,".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera Habibu kwa ushindi huu, acha maela yaendelee kutolea watu wapate mitaji ili mamilionea waongezeke.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...